Anakuwa addressed as: Polycarp Cardinal Pengo, sawa na kusema Jakaya President Kikwete.
Au kwa kiswahili: Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo. Polycarp Pengo ni jina lake sawa na wewe Geomos Muulizaswali.
Cardinal ni cheo chake katika Vatican na haswa maswala ya Papa. Lakini kimsingi ni askofu kama wengine ila mwenye cheo cha juu sio kisakrament bali kulingana na Papa apendavyo. Ni kama vile wabunge wapo wa kawaida na maalumu kama rais apendavyo.
Makardinali ni waana wa kifalme wa Kanisa, au Princes of the Church.
Wanavyokuwa addressed: His Eminence Cardinal....... ni kubwa zaidi ya His Excellence.... kwa rais au askofu wa kawaida.
Kwa kifupi Cardinal ni mtu mkubwa sana ndani ya Kanisa Katoliki na wanahusika kwa karibu zaidi katika uongozi wa Kanisa ikiwa ni pamoja na kumchagua Papa.
Wanaongoza idara kubwa za Kipapa Vatican, ila siyo lazima awe Kardinali hata askofu wa kawaida tu.
Kumbuka Kanisa Katoliki lina waumini zaidi ya millioni 1200 duniani, hivyo Kardinali ni kiongozi wa watu wengi sana kuliko viongozi wa nchi kama USA, China, n.k.