Makosa tunayofanya wasailiwa kipindi cha usaili written or oral interview utumishi

Logi

Member
May 2, 2018
46
200
Kama mada inavojieleza makosa baadhi Yanayotutoa kwenye placements kwa uzoefu mkubwa wangu ni huu

Kipindi cha written interview
1 . Wasailiwa baadhi husahau vyeti vyao vya qualifications bila hivo hutaruhusiwa kufanya usaili

2 Kama ni kada ambazo unahitajika kujisalia kwa mamlaka husika hakikisha unavo vyeti mfano CPA kwa Kada za manunuzi, kwa Engineer ERB Certificate n.k kama kimeisha muda wake jaribu kuwasiliana na board husika wakupe barua ya kurenew la sivyo hautaruhusiwa kufanya interview utaharibu nauli bure

3.Wahi mapema kwenye usaili maana Pia kuna mabadiliko ya ratiba huwa yanatokea la sivyo utapaniki bure jaribu pia Kama umeitwa usaili pitia UTUMISHI WEBSITE siku mbili kabla kuona kama venue imebadilishwa au Laah maana kuna mabadiliko hua yanatokea

4.Kipindi cha usaili jibu short and clear kama ni explain just explain hawana muda wa kusoma easy kama mention just mention usione uko Sharo utanishukuru badae usiwe deep kitu ujaulizwa dakika arobaini ni chache mno usipokua makini zitaisha kwa maswali mawili tu .

Oral interview

1. Protocol ni ile ile wahi mapema lakini usisahau sweta pale kuna upepo na baridi mno kama siku ya kwanza unaweza kutetemeka kwa baridi unaingia usaili kumbe ni hali ya hewa

2. Concentrate ulichokisoma kuna watu pale wako deep lakini confidence zero wakiwa ndani mule usiwe muoga ujui Mungu kakupangia nini?

3.Tambua uwezi kukosa swali la explain about yourself and your background Jitahidi kulifanyia kazi ukikosea hapo hayo mengine huwezi kujibu kwa ufasaha tambua una dakika 20 tu za oral maswali either matano au manne

3. Jiamini ukiona swali hulielewi uliza arudie kuuliza Pia ukiona huelewi au point haziji mwambie skip utajibu ukimaliza hayo mengine

4. Ukitoka kwenye usaili pita moja kwa kwenye kwenye bajaji sepa la sivyo utampa adui silaha ya kukuangamiza tambua upo vitani nadhani nimeeleweka

5. Tambua kupata au kukosa ni majaliwa na bahati Pia kwa sisi watoto wa maskini lakini kwa wenye uhakika sio tabu kwao
Nasisitiza # MATOKEOYA ORAL NI HAKI YETU TUNAHITAJI KUYAJUA PIA KAMA TUNAVO ONA YA WRITTEN#

6. Nasisitiza usiwaogope wasaili maana ni binadamu kama sisi jiamini naimani utajibu vizuri swala la kupata placement muachie Mungu tu kama imefika binadamu hawezi zuia

By Logi
Placement soon will be available be patient
 
Kuna MTU amewahi kufanya interview ya examination officer Secretariat ya ajira? Naomba dondoo.
 
Hii inanikumbusha mwaka 2011 nimemaliza chuo tu nkaomba kazi chapu within interval ya week nkaitwa sehemu mbili tofauti Arusha na dar nkaona nianze ya mbali chap nafika Arusha nko mwenyewe nkapita bila kupingwa tulishia kupiga story nkapewa mda wa kurudi kujiandaa kwaajili ya kazi nlivyorudi kesho yake natikiwa niende intervidw ya dar nlivyoshuka kwa bus nlienda eneo husika kufanya survey ya mazingira then home asubuhi nawahi nkakuta na jam ya hatari njia ya makongo mwenge kipindi hicho kulikua na ujenzi wa barabara nkachukua boda ile nakaribia eneo husika nkapata bonge la ajali shati halitamaniki plus michubuko ya kutosha sikukata tamaa nlirudi mwenge nkanunua shati na kwenda kwenye interview na vidonda vyangu written nkatoboa na oral ni siku hiyo nkaingia na vidonda vyake nkakutana na kabinet imeshiba profs wanne plus drs watano swali tusibitishie wewe so kibaka walinipanikisha then ndo yakaanza maswali ya interview nliwanyosha kiasi walijisahau wakapiga makofi nashukuru nlipata.Arusha nliwapa mtu mwingine
 
Kama Kuna mtu amewahi kufanya interview ya ya katibu wa afya tunaomba sample ya maswali
 
Hongera sana mkuu. Hii ndio maana halisi ya "mpaka tone la mwisho " infact you deserved this one

Pia ulitisha kwa kua na moyo mkunjufu kutoa pande kwa wengine iyo position ya Arusha ingekuwa mwingine angepuuzia na asingejali kushare na wana.

Funzo Kubwa: Don't Give Until the last Breath.
 
Back
Top Bottom