Makosa SUMATRA inayafanya kuelekea tiketi za electroniki

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,602
Habari wanajamvi,
Mimi kama mdau wa Teknohama nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mabadiliko ya nchi kuelekea mifumo ya kielektroniki. Kuna kitu nimekiona hakiko sawa na ningependa kukiweka hapa. Ninakiweka hapa kwa lengo moja tu, nalo ni kuhakikisha wahusika wanalifahamu. Hii ni kwa sababu nchi yetu mpaka sasa haina utaratibu wa kualika wadau wa sekta ya Teknohama ili kupata maoni na ushauri wao katika masuala anuai yanayohusu sekta hii.

Tangazo lililoenea mitandaoni hivi karibuni limeonesha SUMATRA wanaanzisha utaratibu wa kutumia tiketi za kielektroniki kuanzia mwakani. Details za tangazo la SUMATRA zinapatikana hapa kwa wale ambao hawakuliona. Nikiwa kama mdau wa sekta hii ya Teknohama na ambaye nimefanya hizi kazi za tiketi za kielektroniki nje ya Tanzania naona kuna kosa SUMATRA wanaelekea kulifanya ambalo si afya kwa Taifa.

Kulingana na maelezo yao, inaonesha SUMATRA tayari wana mfumo wao wanaoupendelea (System of their choice). Hapa nanukuu:

“Kwa sasa tumeanza mpango huo kwa majaribio kwa daladala za kampuni ya Christian, Desemba tutaenda kwa mabasi ya mikoani na Januari mwaka kesho, mfumo huo utaanza kwa mabasi na daladala zote,” alisema Kahatano.

Hili kwangu mimi naona ni kosa kitaalam. SUMATRA ni wasimamizi na hawapaswi kuwa na mfumo wanaoupendelea au kuuonea. Hii ni kwa sababu Mifumo ya tiketi ni biashara kama zilivyo nyanya na vitunguu. SUMATRA akiwa kama mwakilishi wa serikali alipaswa kutoa mwongozo na vigezo vya mifumo husika kisha watu wakaunda mifumo yao na kuipeleka SUMATRA kwa ajili ya kupitishwa kama imekidhi vigezo. Hivyo ndivyo nchi zingine ninazozifahamu zinavyofanya ikiwemo majirani zetu wa Kenya na Rwanda.

Mamlaka husika zinafanya vetting ya makampuni na mifumo yao na kila mfumo unaopita katika chujio basi unakuwa approved na unaruhusiwa kutumika na mabasi/daladala. Hii ni kwa sababu wamiliki wa daladala na mabasi wanapaswa kuchagua mtoa huduma wanakayemtaka kwa bei ya huduma watakayokubaliana na si kulazimishwa kwa kuweka chaguo moja au mawili.

Kitendo cha kuupa mfumo mmoja upendeleo si jambo zuri na litadumaza ubunifu na kupelekea huduma mbovu (kwa sababu ya monopoly). Nawashauri SUMATRA wapitie upya uamuzi wao na badala yake waweke vetting procedures ili wao wabakie kama refa asiye na upande. Wao wabakie kama regulators na wasimamizi wakuu wa hii mifumo.

Wakifanya hivyo itachochea ubunifu na kuongeza ajira wakati huu ambapo ajira ni changamoto.

Kwa kufunga maoni yangu niishauri serikali iwe inawashirikisha wadau wa maeneo ambayo inataka kufanya mabadiliko makubwa ya kitaalam. Hii nchi ina watu wengi walio tayari kutoa ushauri kama wakitaka.

Wasalaam!


Addendum: Kuna swali ambalo linaweza kuja kwamba SUMATRA wataweza vipi kusimamia let say mifumo 20 tofauti? Kifupi ni kuwa katika Technical Specs za mifumo lazima kuwe na kipengele cha Unified Monitoring API/UI ambapo System husika itapaswa kuji integrate na Monitoring System ya SUMATRA.
 
Back
Top Bottom