singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SHERIA za Makosa ya Mtandao na Miamala ya Kielektroniki ya Mwaka 2015, imesaidia kupunguza makosa ya mtandao kwa asilimia 60 tangu kuanza kutumika Septemba mosi, mwaka jana.
Hatua hiyo imetokana na wananchi kuanza kuelewa matumizi bora ya mitandao na kuwezesha matumizi ya mtandao kutumika kwa jinsi ilivyokusudiwa .
Hayo yalisemwa jana katika kikao cha kujadili sheria hiyo kwa wafanyakazi na walimu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kilichofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Kitendo cha Sheria katika wizara hiyo Kitengo cha Mawasiliano, Veronika Sudayi alisema kati ya makosa yaliyokuwa yameshamiri na sasa kupungua kwa kiasi kikubwa baada ya kuanza kutumika sheria hiyo ni picha za ngono mitandaoni, makosa ya udhalilishaji watoto na watu wazima.
Sudayi alisema kuna makosa ambayo bado yanaendelea kwa kasi mitandaoni yanayohitaji kuchukuliwa hatua stahili ikiwemo elimu kwa umma ambayo ni uchochezi na taarifa za uongo unaofanywa na kundi kubwa la vijana.