Kifurukutu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 4,628
- 6,669
Salamu wakuu!
Kwanza napenda kutambua juhudi za kikosi cha usalama barabarani na jeshi la polisi kwa ujumla katika kukamilisha majukumu yao kupunguza ajari barabarani na kuongeza ufanisi katika matumizi ya barabara, kuongeza makusanyo ya mapato yatokanayo na makosa ya vyombo vya usafiri,
pia kitendo cha kuweka tochi dhibiti mwendo kwa madereva barabarani ni hatua kubwa kwa serkali na jeshi la polisi usalama barabarani.
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana pasi na majibu ya kujiridhisha, nimeonelea Jf naweza pata majibu mujarabu na wahusika wakajirekibisha pia kupitia mawazao yenu.
Hivi hizi sheria za barabarani zimewekwa kwa ajili ya wamiliki wa vyombo vya moto binafsi tu?
Inakuaje askari wa usalama barabarani hawahusiki na uvunjwaji wa sheria barabarani unaofanywa na magari ya serikali? Au ndio kusema magari ya serikali hayavunji sheria?
Kwamba tochi za barabarani hazioni gari za serikali zikikimbia zaidi hata ya speed 120km/h sehemu inayoitaji speed ya 50km/h na wazipige faini?
Ni rai yangu sasa kwa jeshi la polisi kuanza kufuata haki na usawa, sheria zinazotumika lwa magari binafsi zitumike pia kwa magari ya serikali!
Nawasilisha