samahani ni kuwa makontena yameibiwa au ni makontena yamepita bila kulipiwa ushuru.Kuna kitu hapa cha kuweka sawa unapozungumza makontena yamepotea inamaana hayajulikani yalipo kabisa.Ila unapozungumza yamepita bila kulipiwa ushuru ina maana mwenye kontena anajulikana ila hakulipa mapato ya serikali.Jamani tuweke Kiswahili sawa kusaidia mwananchi wa kawaida kuelewa
samahani ni kuwa makontena yameibiwa au ni makontena yamepita bila kulipiwa ushuru.Kuna kitu hapa cha kuweka sawa unapozungumza makontena yamepotea inamaana hayajulikani yalipo kabisa.Ila unapozungumza yamepita bila kulipiwa ushuru ina maana mwenye kontena anajulikana ila hakulipa mapato ya serikali.Jamani tuweke Kiswahili sawa kusaidia mwananchi wa kawaida kuelewa
Hiyo meli ilyoingia ilikuwa (kulingana na habari yenyewe) ina uwezo wa makontena 250-300 ya 40ft au mara mbili ya idadi hiyo 500-600 ya 20ft.hivi meli moja ina uwezo wa kubeba makontena mangapi??
Nchi ya mazezeta hii lazima iliwe tuHawa wanahangaika bure, muhusika mkuu yupo kijijini wilaya ya Bagamoyo anakula kiyoyozi tuu anacheki watu wanavyo ZOZA tuu
Acha kutia watu presha aisee, kwanza keshastaafu!
Wenye kukijua kiswahili vizuri watakuja kuweka sawa ila kwa hili siyo jipya na kilichopo hapa ni ushuru ndiyo haujalipwa na wanajulikana.
Mabosi wengi sana wanajua haya mambo. Kama huyu aliyestaafu... Kova atakuwa alikuwa mhusika! Lakini kwa vile anajua madhambi, u-comedy na uongo aliokuwa anatumwa na serikali na CCM kufanya kwa manufaa yao hawatakuwa na nguvu ya kumtikisa! Ndio hasara ya kutumia polisi kupinda mambo kwa faida ya watawala.Katika gazeti la la Raia Tanzania, habari ya " Meli yaibwa" , habari iliyopo ukurasa wa nne, mwandishi katumbua jipu.
Katika habari hii mwandishi kaandika kwa kina juu ya uhusika wa TPA na TRA kutorosha makontena toka bandarini hivyo kukwepa ushuru na mapato ya bandari.
Hata hivyo kitu cha kushitua ni uhusika wa Kituo cha Kati cha Polisi (Central Police).
Katika paragraph moja, nanukuu:
"Raia Tanzanialilithibitishiwa kufanyika kwa mchezo huo(kupitisha mizigo ya meli nzima bila kulipia ushuru na mapato ya bandari) zaidi ya mara moja ukiwahusisha maofisa wa TPA, TRA na Kituo cha Kati cha Polisi)"
"Kinachofanywa na polisi ni kuzua tatizo bandarini na kujifanya wanafuatilia tatizo hilo lisilokuwa na kichwa wala miduu, kumbe ni katika kurahisisha 'deal' za namna hiyo. Wanafahamika kwa majina maofisa wa polisi waliokuwa wakihusika"
Haya inasemekana yametonywa na mtu toka ndani ya TPA, kulingana na gazeti hili la Raia Tanzania.
Haya wadau , jipu hilo ndani ya jeshi la Polisi!
Mkuu kama kuna polisi alihusika kuvunja sheria basi its on his/her personal capacity, na mtu ahukumiwe hivyo.Mabosi wengi sana wanajua haya mambo. Kama huyu aliyestaafu... Kova atakuwa alikuwa mhusika! Lakini kwa vile anajua madhambi, u-comedy na uongo aliokuwa anatumwa na serikali na CCM kufanya kwa manufaa yao hawatakuwa na nguvu ya kumtikisa! Ndio hasara ya kutumia polisi kupinda mambo kwa faida ya watawala.
Inaelekea kweli.....!Majambazi kabisa...