masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Katika gazeti la la Raia Tanzania, habari ya " Meli yaibwa" , habari iliyopo ukurasa wa nne, mwandishi katumbua jipu.
Katika habari hii mwandishi kaandika kwa kina juu ya uhusika wa TPA na TRA kutorosha makontena toka bandarini hivyo kukwepa ushuru na mapato ya bandari.
Hata hivyo kitu cha kushitua ni uhusika wa Kituo cha Kati cha Polisi (Central Police).
Katika paragraph moja, nanukuu:
"Raia Tanzanialilithibitishiwa kufanyika kwa mchezo huo(kupitisha mizigo ya meli nzima bila kulipia ushuru na mapato ya bandari) zaidi ya mara moja ukiwahusisha maofisa wa TPA, TRA na Kituo cha Kati cha Polisi)"
"Kinachofanywa na polisi ni kuzua tatizo bandarini na kujifanya wanafuatilia tatizo hilo lisilokuwa na kichwa wala miduu, kumbe ni katika kurahisisha 'deal' za namna hiyo. Wanafahamika kwa majina maofisa wa polisi waliokuwa wakihusika"
Haya inasemekana yametonywa na mtu toka ndani ya TPA, kulingana na gazeti hili la Raia Tanzania.
Haya wadau , jipu hilo ndani ya jeshi la Polisi!