donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,257
- 22,138
Salam wakuu,
Kwa muda wa miaka mingi enzi za zamani, ukitaja katika shule ambazo zilikua zinafanya vizuri kitaaluma na kimichezo, makongo nayo ilikuepo kwenye list. Nakumbuka enzi za headmaster Col Iddi Omary Kipingu, alijitahidi kuiweka makongo katika ramani ya kimichezo na kitaaluma. Ni wanasport wengi sana ambao wamepitia shule ya sekondari ya makongo ambao waliwika au wanawika katika nyanja za michezo mbali mbali. Nakumbuka wimbo wa shule kidogo," Najivunia shule yangu makongo, sekondari ing'aayo kielimu, pia na kwa fani nyingine zote makongo sekondari oye oye". Enzi hizo ukitaka uone cha mtema kuni kutoka kwa marehemu afande miraji au babu chacha basi wewe uchelewe asembo au usiwe unaimba wakati wenzako wanaimba. Wapi wale wazee wa JORO? Hiki kilikua ni chakula cha wabishi peke yake. Kiukweli shule zamani ilikua ina perfomance nzuri tu, lakini kwa miaka ya karibuni hali imebadilika sana. Makongo sasa hivi imekua mdebwedo sana kuliko hata baadhi ya shule za kata. Imagine kama mwaka jana division one kidato cha nne ilikua moja tu..!! Nashindwa kuelewa what went wrong mpaka shule imefikia kushika mkia kiasi hiki. Anyways, kwa wale ex-makongo je nio kitu gani unakikumbuka zaidi pale makongo? Au ni adhabu gani ambayo ulishawahi kuipata ambayo kamwe hautoisahau? Nawasilisha.
daaaa kaka umenikumbusha mbali sana "nidhamu ndio mafanikio yetu........makongo oyeee elimu ni msingi" serious tangia Mh Kipingu aondoke makongo imekuwa historia, Marehemu Miraji, Marehemu Yeyee, Afande Babu chacha na wengineo walitutengeneza aswaah, tangia apewe shule mwaseba ndio mambo yalipoanza kufulugika. Ikawa shule ya kuangalia fedha kwanza ili mtu ajiunge na sio uwezo. NITAIKUMBUKA NA KUIPENDA SANA MAKONGO YANGU YA MWAKA (2000-2004)
Dah umenikumbusha babu chacha mzee wa ku-love ahahaha kumbe Miraji nae alimfuata yeyeye wapumzike kwa
amani peponi.
Ha ha ha daaah nakumbuka kipindi kile nisipojisikia kukaa class naenda zangu Nyambiz hall kupiga buku......lol Yeye alikuwa na kelele ile mbaya,Wapi Kisarika ni noma mbayaa,Mataula kitu black ile mbaya.
Makongo enzi ile bwana........
Ugari wa afande said, ugali wa wachezaji wa timu ya vijana,miaka ya 97, 98, na 99, makongo ilikuwa baraha kwa kila kitu, tuliomaliza mwaka 1999 na matokeo kutoka mwaka 2000 palikuwa na div 1 - 76, kwa sasa n up.upu mtu,
Unamkumbuka afande Yeyeye?
Hahaa aloo umenkumbusha mbali sana, me bana sintosahau afande blusi wa mabweni ya wavulana alinkuta room mida ya class nili dodge, alinipa adhabu ya kuruka kichurachura niuzunguke mti mara 50,
Aftr those rounds sikuweza simama kabisa misuli iligoma hadi nkakandwa na ice,
"makongo ooye elimu ni ulinzi"
2004-2007
Aisee kisarika na sura yake kama mchina akikukamata jiandae kupata shurba kali sana. Ole wako usije zamu, utamjua afande miraji ni nani.
Hahaa aloo umenkumbusha mbali sana, me bana sintosahau afande blusi wa mabweni ya wavulana alinkuta room mida ya class nili dodge, alinipa adhabu ya kuruka kichurachura niuzunguke mti mara 50,
Aftr those rounds sikuweza simama kabisa misuli iligoma hadi nkakandwa na ice,
"makongo ooye elimu ni ulinzi"
2004-2007
Daaah umenikumbusha mbali sana.Kipindi cha ramadhan nakumbuka watu walijua kwa kuwa alikuwa katika mfungo asingeweza weza waadhibu watu, siku hiyo ilikuwa balaa marehemu afande Miraji aliwachezeshea watu kipigo ambao hawakuja zamu za kufanya usafi kipindi cha likizo siku hiyo walilia wengi sitoweza isisahau siku hiyo tukiwa form two. Rest in peace, Afande Miraji.
Wapi Mwashiga....,Mr Mayebe a.k.a Masta,wapi Nyalusi.....,Madeghe,....,Malongoli....,Mgongolwa.....,Kaimbe....,Mchwampaka.....,Kombaa mwalimu wa French!!!!!
Mr Mayebe a.k.a Masta huo moto ogopa sana ni hatariii, Siku moja nikachelewa ilikuwa zamu ya asubuhi class kwetu kuna teacher nikadivert nikiogopa kuchezea, si nikazama darasa la watu ambalo lilikuwa hakuna mwalimu kumbe mule nilipoingia masta ndo alikuwa anakipindi, akazama akaanza fundisha harafu kama jana yake alikuwa amewapa home work, akaanza kagua kwa kila mmoja du bahati nzuri alipitiwa hakunitazama lakini mi moyoni ilikuwa balaa.