Makonda wa daladala na majibu yao.

Makonda wa daladala na majibu yao.

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,034
Nilipanda hiace tokea dumila kwenda moro.Mara njiani tukampakia mama wa kimasai akiwa na mwanawe kichanga,alikosa seat hivyo alisimama.Ile hiace ikaendelea kuokota abiria njiani.Yule mama wa kimasai akaanza kulalama,"we konda,hapana ongesa mutu ingine,mutoto yangu naumia!".Konda akajibu,"aah!mama,wewe ng'ombe wako chuchu zikijaa maziwa mpaka yanavuja unachekelea kweli,na sisi gari ikijaa mpaka mkisimamia mguu mmoja mmoja tunafurahi pia!",kwa hiyo piga kimya.
 
ABIRIA: konda usiongeze watu gari limesha jaa
KONDA: sheria za nchi zipo kibao nawewe unaleta za kwako tena!
ABIRIA: Sitaki siti za nyuma kuna joto
KONDA: aaah mpango gani sasa huo,kama vipi si ukapande friji !
 
teh teh teheeeee
 
Ccta 1 alipanda kwenye tax uch(kama alvyozalwa)dereva akawa anamshangaa,ccta akamuulza mbona unanshangaa hujaw kuona uch,dereva akajb cshangai uch wako ila nawaza hela za kunlipa utakuwa umeweka wapi?
 
abiria: siti zipo
konda:siti zipo ila zimekaliwa zote..
 
Mama mmoja alichungulia kwenye daladala na mazungumzo yakawa hivi:

MAMA: Wee konda kuna seat kwenye gari?
KONDA: Ndiyo zipo.
Mama akataka kupanda, lakini akakuta seat zote zimekaliwa na watu. Ikawa hivi:
MAMA: Wee konda vipi, mbona unasema kuna seat wakati hakuna.
KONDA: Wee mama vipi, hizo seat walizokalia watu huzioni? Hili ni gari sio ngalawa, kwa hiyo ni lazima liwe na seat. Hujaniuliza kama kuna seat zilizo wazi.
 
ABIRIA; We konda huoni gari imeshajaa? Kutafutiana magonjwa tu...
KONDA; kama unataka starehe kakodi TAX
 
Ccta 1 alipanda kwenye tax uch(kama alvyozalwa)dereva akawa anamshangaa,ccta akamuulza mbona unanshangaa hujaw kuona uch,dereva akajb cshangai uch wako ila nawaza hela za kunlipa utakuwa umeweka wapi?

MKUU, hivi upo chuo gani ili nami nije kupata huu ujuzi wa kufanya jokes??
 
Abiria: konda kuna siti?
Konda: kwa hiyo hao walio kaa wamekalia vigogo?
Sister du: konda unanibana.
Konda: mbona hiyo suruali uliyo vaa inakubana halafu huisemi?
Abiria: konda weka nyimbo za Yesu.
Konda: Yesu hajatoa album.
 
Back
Top Bottom