Makonda usipoteze muda wako

Makonda usipoteze muda wako

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,095
Reaction score
79,493
WANAWAKE HUENDEKEZA KUTAPELIWA.

Na, Robert Heriel.

Mtu anayefuata sheria na utaratibu kamwe hawezi kutapeliwa. Hasa sheria na amri za Mungu. Anayefuata mila na desturi kamwe hawezi kutapeliwa. Ukisikia mtu katapeliwa basi jua kuna sehemu amevunja sheria za dini au mila na desturi.

Moja ya Sababu ya mtu kutapeliwa ni tamaa na kutofuata taratibu za jambo husika. Ni ile tabia ya uasi na kufanya mambi kisiri siri.

Suala la mapenzi lisiwe suala la siri kwa vijana waliofikisha umri wa kuoa au kuolewa. Unakuta mtu anamiaka 20+ anaogopa kumuita kijana anayemchumbia nyumbani kwao ili wazungumze nyumbani.

Binti anamficha Mama yake kuhusu mambo ya mahusiano yake. Bado asitapeliwe thubutu. Mambo ya kimya kimya ndio huzaa utapeli.

Wewe binti kama umefikia umri wa kuolewa na kijana amekufuata na unampenda. Unashindwa kumuuliza kuwa je hajui utaratibu. Kama hajui mwambie utaratibu ukoje. Mwambie aandike barua iende kwa wazazi. Kisha taratibu zingine zifuate. Aje kwenu nawe uende kwao. Kisha mtangaze ndoa kwa siku kadhaa kuona kama kuna pingamizi. kama hakuna fungeni ndoa.

Sasa jitu linafanya mambo kimya kimya kwa nini lisitapeliwe. Mtu hataki hata kukuweka Profile picture wewe unachekelea tuu kama mwehu. Mtu anataka ndoa ifungwe kimya kimya hushtuki tuu kuwa kuna wizi unaendelea. Unakuja kuolewa baada ya miezi kadhaa unashangaa mke mwenzako anakuja kukutoa. Ati unalia. Pumbavu wewe ni wa kuchapa bakora. Unadanganywa kama mwehu.

Alafu shida nyingine ni kuwa vitoto vya siku hizi inajifanya inajua kila kitu. Haitaki ushauri kwa wazazi na wakubwa zao. Ati wameenda shule. Shule gani kama sio upuuzi. Mwishowe inakuja kusumbua watu.

Vijana nao kazi ujinga. Unahonga pesa kama kichaa. Ati ninasomesha. Mara ninamhudumia. Unamhudumia ni mke wako huyo. Akikuacha unaona watu wabaya wakati wewe ndio akili yako ni saa mbovu. Kutapeliwa ni kukiuka sheria za msingi. Mke ndio huhudumiwa hao wengine fukuza huko.

Mhe. Makonda hao unaowatetea kuwa wanatapeliwa ndio wanaoendekeza huo utapeli. Wao ndio wanataka watapeliwe. Ukiona mtu katapeliwa ujue yeye ndio chanzo cha huo utapeli.

Najua inakuumiza kuona Dada zetu wakilaghaiwa hali inayopelekea kupewa mimba na kutelekezwa. Hali inayopelekea Kuwatumikia wanaume kinyumba kwa miaka kadhaa alafu mwishowe hufukuzwa kama Paka shume. Ni kweli inauma lakini nakuhakikishia kuwa Chanzo kikubwa cha wao kulaghaiwa ni wao wenyewe kutaka.

Mwanamke aliyefunzwa akafunzika kamwe hawezi kulaghaiwa na mwanaume. Hawezi shindwa kujua yupi ni mwanaume mkweli na yupi ni mwanaume Muongo.

Mwanamke akitapeliwa ni wazi amejishusha viwango vya kuwa Mke mwema ndani ya nyumba. Ni wazi hatakuwa Mama Bora ingawa anaweza jifunza kutokana na makosa lakini ni wachache wanaojifunza kutokana na makosa.

Mhe. Makonda unaposema ndoa zisajiliwe sijajua unazungumzia nini. Mimi ninachojua ni kuwa ndoa ni lazima iwe imesajiliwa. Iwe ni ndoa ya kidini, Kimila au Ndoa ya serikali. Bahati nzuri ni kuwa mwenye mamlaka ya kusajili ndoa ni Serikali na ndio inayotoa vyeti. Sasa hizo ndoa unazosema zisajiliwe ni zipi.

Kama ni zile ndoa za kihuni za njoo tuishi pamoja hizo sio ndoa. Hizo ndizo huleta athari mbaya na hata kufikia watu kufanyiana utapeli.

Mhe. Makonda tamko lako lingetakiwa kusema Wale ambao hawajagunga ndoa ya aina yoyote lakini wanaishi pamoja waende mahala husika wakajisajili. Na ungependekeza bunge liunde sheria ya kuwa ni marufuku kwa mwanaume na mwanamke wasio na undugu kuishi pamoja bila kufunga ndoa. Kisha iwekwe adhabu kali kwa watakao kiuka.

Sheria hii ingekuwa na manufaa mengi. lakini faida kubwa ni kuwa na taifa lenye maadili ya kibinadamu na sio taifa la watu wanaoishi kama wanyama ambalo mtu akitaka kuishi na mwanamke/mwanaume anaishi tu bila wasi wasi. Hiyo ni desturi ya Wanyama.

Pia sheria hii itaongeza mapato ya taifa kwani Wanandoa watatoa pesa ya Vyeti au namna yoyote ile ya usajili.

Mhe. Makonda nature ipo wazi kabisa kuwa Mwanaume ndiye mtawala na ndiye muwindaji. Wakati mwanamke ni mtawaliwa na muwindwaji. Hao wanawake unaowatetea kuwa wanatapeliwa ni kutokana na kukiuka nature. Wanawake wanapaswa kutozurura zurura hovyo. Lakini wanawake wa siku hizi kutwa kiguu na njia tadhani wao ni wawindaji. Kutwa kwenye kumbi za starehe ilhali wao ni wawindwaji.

Wanawake wanapaswa kukaa ndani na kama watatoka iwe ni kwa sababu maalumu hasa hasa kazini. Lakini wanawake wa siku hizi ni kama wanaume kutwa kuzurura na hapo ndipo hukutana na wanaume mafisi na simba wala nyama. Jambo hili litokea ndipo kizaa zaa huzuka. Hata Hawa/Eva alianguka kwa Kuzurura hovyo bila mpango. Alisahau yeye ni muwindwaji.

Mhe. Makonda hao wanawake wa siku hizi wanaotapeliwa wanataka wenyewe kutapeliwa. Unakuta limwanamke halifanyi kazi. Livivu kutwa kuomba omba pesa kama omba omba asiye na miguu wala mikono. Wenyewe siku hizi wanaita kudanga. Hivi Mkuu Makonda kwa akili yako Mvuvi anapoweka Chambo kwenye ndoano unafikiri anadhumuni gani. Mvuvi anajua kuwa wapo samaki wenye uroho watabwia chambo kwa ulafi wao.

Wapo wanawake wengi siku hizi wenye uroho wa pesa. Na wanaume kama wawindaji kwa kujua jambo hili huweka pesa kama chambo kusubiri Wanawake wenye uroho. Hapo ndipo utapeli hutokea.

Ningefurahi kama ungepiga marufuku kwa wanaume wote kutoa pesa au mali yoyote kwa wanawake ikiwa sio wake zao au ndugu zao. Hapa ungecheza kama Ronaldo. Lakini unazuia upande mmoja alafu upande mwingine unaachia. Hata hivyo mambo haya ni mambo binafsi lakini kama umeamua kuyaingilia ni sawa. Usizuie upande mmoja zuia pande zote.

Mhe. Makonda najua huna lengo la Kupambana na jambo hili. Na kama unalengo basi nakusihi fuata ushauri wangu kama ifuatavyo;

1. ZUIA HAKUNA MWANAMKE KUOLEWA BILA BIKRA.
Zamani hapakuwa na utapeliwa kwani kulikuwa na sheria kali. Mwanamke alipaswa kujitunza na wazazi wa mwanamke walihakikisha aibu haiwapati. Walimtunza binti yao.

Ikiwa utatoa tamko kuwa mwanamke asiolewe bila bikra. Nakuhakikishia hutasikia habari za utapeli wa mapenzi. Hutasikia habari za wanawake wanaozaa kabla ya ndoa ambalo kwa sasa ni janga kubwa sana.

Hutasikia habari za Wanaume wenye vibamia. Hutasikia habari za Baba wa Kambo au mama wa kambo. Hutasikia mambo ya Ex wangu. Hutasikia hayo nakuhakikishia.

Bunge liunde sheria hiyo kama taifa linataka liwe sirius na masuala haya. Vinginevyo unapoteza muda wako.

Katika hili Natarajia changamoto kubwa kutoka kwa Wanawake wengi ambao wameshatoa bikra zao. Hilo lisiwe sababu hao wataolewa na wazee ambao wake zao wamefariki.

2. Dhibiti nyumba za Wageni na Nyumba za kupangisha.
Mwanamke na mwanaume wasiingie nyumba ya wageni ikiwa hawana vitambulisho vya ndoa. Hii itazuia zinaa na uasherati. Mmiliki wa Guest kama atakiuka sheria hii basi atafutiwa kibali cha kuendesha biashara hiyo

ingawa itafanya biashara ya Nyumba za wageni kuwa ngumu lakini itajenga maadili ya taifa.

Halikadhalika na upande wa Nyumba za kupangisha. Asipange mwanamke na mwanaume kwa pamoja kama sio wanandoa na kama hawana vitambulisho vya ndoa.

3. Mgawanyo wa Shule.
Pawepo na shule za Wasichana na shule za Wanaume pekee yao. Shule za wanawake wafundishe waalimu wa kike pekee. Halikadhalika na shule za wavulana wawepo waalimu wakiume tuu.
Miaka ya Shule za sekondari na shule ya msingi ipunguzwe angalau mwanafunzi amalize kidato cha sita akiwa na miaka kumi na sita

Chuoni pawe na mchanganyiko chini ya uangalizi mkali. Chuoni pawe ndio sehemu ya vijana kutafuta wachumba chini ya uangalizi wa Mshauri wa Wanafunzi.
Hii inachangamoto nyingi lakini sababu za huko juu zitaifanya ifanye kazi hasa mtoto wa kike kutokuolewa endapo hatakuwa na bikra.

4. Sheria na adhabu kali kwa Watakaokiuka.
Serikali iunde sheria kali kwa watakaokiuka amri hizo. Iwe ni mwanamke au mwanaume.

Kama binti atakutwa na kijana wakifanya mapenzi wapewe adhabu kali ikiwezekana kufungwa kifungo kisichopungua miezi sita kwa mwanamke. Na kisichopungua mwaka mmoja kwa mwanaume.

Miezi sita kwa mwanamke kwa kuwa yeye atakuwa kapoteza bikra na hataolewa na vijana bali wazee. Zaidi ya mwaka mmoja kwa Mwanaume kwa kuwa yeye hana alichopoteza na ataoa mwanamke amtakaye

5. Kifungo cha miaka thelasini kwa Mtu atakayechepuka ndani ya ndoa.
Hii iwe kama kwenye kesi ya ubakaji. Mwanaume au mwanamke atakayechepuka ndani ya ndoa afungwe miaka thelasini.

Uone kama taifa halitanyooka hili. Ukiona uovu unaenea kwa kasi ujue Watawala ni mawakala wa Shetani. Hivyo ndivyo ilivyo.

Ni hayo tuu kwa Leo.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi
0693322300
 
Tuache maji yafate mkondo wake, ndoa za lazima zitazaa matezo na utumwa. Ni bora aliyetoweka mapema kabla ya kuketa usumbufu ndani ya ndoa.
 
Back
Top Bottom