Makonda Shukran Sana; Ila visu, bisibisi, nyembe, vimeshamiri Mitaani

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,188
7,490
Mheshimiwa RC Makonda nakusalimu, naamini unaendelea vyema na shughuli za ujenzi wa taifa hili.Kwanza nikupongeze kwa jinsi unavyoonesha jitihada zako katika kulibadili jiji la dar ili iwe sehemu nzuri zaidi ya kuishi. Binafsi huwa navutiwa sana na juhudi zako na mimi ni miongoni mwa wanaokuunga mkono.

Mheshimiwa shukurani zetu za ziada kwako, ni kwa hili la kusaidia PF-3 zipatikane kwa urahisi ili watu wanaoumia waweze kutibiwa kwa wakati na bila usumbufu. Hata hivyo wananchi wako hatuna raha wala amani kabisa mitaani!

Mheshimiwa, Sijui kama unafahamu kuwa huku mitaani kuna watu wanatuchoma na mabisibisi, visu, nyembe na vitu vingine vyenye ncha kali? jambo la kusikitisha ni kwamba vitendo hivyo hufanyika hadharani tena mchana kweupee? na wanaofanya hivyo wanafahamika mpaka na watoto wadogo ila hakuna hatua inayoonekana kuchukuliwa na watu hao wapo mahali palepale pale wakifanya matukio yale yale na wakijeruhi watu kila siku.Linalohuzunisha zaidi ni kwamba haifahamiki kwamba watu hao hutumia kitu chenye ncha kuchomea wananchi wangapi kwa siku !

Mheshimiwa; watu wanaofanya matendo hayo, wapo wazi kabisa,wanafanya hadharani, wakati wa mchana hujipanga kwenye vituo vya dalala dala wakijifanya wanapiga debe, huku wakiwalazimisha makonda kutoa kiasi fulani cha fedha na wasipotoa, au wakitoa kiwango tofauti huwachoma na vitu vyenye ncha kali!. Kwa upande wa abiria huwapokonya simu, vipochi na hela na kukimbilia sehemu zinazofahamika ambapo wanakaa kwa makundi.Watu hao hao usiku ndio huingia mitaani na kuwavizia wananchi, kuwajeruhi na kuwaibia au kukimbia.

Mheshimiwa; wakazi wa dar hatukai kwa amani kwa sababu ya wapuuzi hawa ambao wanaonekana kutamba kwa miaka sasa! kwa kuwa wahuni hao wanafahamika na kwa kuwa tunaamini uwezo wa kuwadhibiti upo, tunaomba pamoja na lile la PF-3, Basi utusaidie na hili mkuu kwani naona una dhamira ya kweli ya kulifanya jiji la Dar kuwa sehemu nzuri ya kuishi. Naamini, mbele ya kiongozi wa aina yako, lolote dar inawezekana isipokuwa kuponguza joto.

Tunatanguliza shukurani zetu,

Raia wako,
Betlehem
kwa niaba ya wengine wanaokerwa na hili.
 
Pia naomba kuwashauri wananchi wenzangu nao kuwa suala la mabadiliko ni suala la kijamii, pamoja na michango ya viongozi katika kuelekea kwenye mabadiliko, jamii nayo ina mchango kamili katika kulifanikisha hilo.Ni vyema kila raia kwa wakati wake akajiuliza; "Ni kwa vipi anatimiza wajibu wake katika kukabiliana na uovu na matatizo yanayoikabili yamii yake".
 
Umeisikia ya NSSF..!? Tenda zinatolewa kama njugu.?
==============================
Kweli Makonda shughulikia hilo.
 
Kwani Makonda ni Polisi? Hayo mambo mwambie OCD,RPC na IGP.Makonda atapiga siasa tu kama zile za PF3 na nauli bure kwa walimu lakini utekelezaji sifuri.
 
Hawa ni zaidi ya majambazi yanayokutandika risasi unakufa hapo hapo.

Sasa hii ya kuchomachoma watu na vitu vya ncha kali ni hatari sana sikuhizi kuna magonjwa mengi sana.

Naunga mkono suala hili liangaliwe kwa undani zaidi.
 
Kwani Makonda ni Polisi? Hayo mambo mwambie OCD,RPC na IGP.Makonda atapiga siasa tu kama zile za PF3 na nauli bure kwa walimu lakini utekelezaji sifuri.
Ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi, ni kama rais wa mkoa, ana uwezo wa kuwaagiza wengine , kufuatilia na kuchukua hatua mbalimbali za kimaamuzi ikibidi.Kinachohitajika kwenye baadhi ya mambo ni utashi tu na dhamira ya kweli mengine yanaenda.
 
Hawa ni zaidi ya majambazi yanayokutandika risasi unakufa hapo hapo.

Sasa hii ya kuchomachoma watu na vitu vya ncha kali ni hatari sana sikuhizi kuna magonjwa mengi sana.

Naunga mkono suala hili liangaliwe kwa undani zaidi.
Kweli kabisa mkuu, yaani inaudhi sana aisee, na ni heri majambazi unaweza kusema kuwa wanafanya kazi zao kwa siri na kwa kushtukiza kisha kutoroka kwa hiyo pengine udhibiti wao ni mgumu kidogo lakini hawa majamaa wanafanya uhalifu mchana kweupee na hadharani kabisa watu wanaangalia tu kana kwamba ni sehemu ya maisha.
 
Sasa NSSF inahusikaje hapa mkuu?
Hicho kilikuwa kibwagizo cha kukuuliza kama umeishazipata habari juu ya nssf....maana nilitafuta sana mchango wako kwenye uzi wa habari hizo bila mafanikio. Baada ya kibwagizo nikaunga mkono hoja iliyokomezani.
 
Ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi, ni kama rais wa mkoa, ana uwezo wa kuwaagiza wengine , kufuatilia na kuchukua hatua mbalimbali za kimaamuzi ikibidi.Kinachohitajika kwenye baadhi ya mambo ni utashi tu na dhamira ya kweli mengine yanaenda.
Ulinzi na usalama ni utaalamu,Makonda hana utaalamu wowote wa kusimamia ulinzi na usalama.Hivyo ni vyeo vya kisiasa tu walivyopewa makada wa CCM ili kuhakikisha wanabaki madarakani kwa njia haramu.
 
Hicho kilikuwa kibwagizo cha kukuuliza kama umeishazipata habari juu ya nssf....maana nilitafuta sana mchango wako kwenye uzi wa habari hizo bila mafanikio. Baada ya kibwagizo nikaunga mkono hoja iliyokomezani.
mkuu? hebu jiulize mtu anakuchoma na sindano baada ya kutaka uumpe sh.1000 bila kufanya kazi yoyote ile na wewe ukaamua kumpa 500 badaya ya 1000 anayoitaka (licha ya kuwa hakudai na hakuna kazi aliyoifanya) halafu sindano aliyokutoboa nayo ina magonjwa mbalimbali ya kuambukiza hivi NSSF ina maana gani?
 
Ulinzi na usalama ni utaalamu,Makonda hana utaalamu wowote wa kusimamia ulinzi na usalama.Hivyo ni vyeo vya kisiasa tu walivyopewa makada wa CCM ili kuhakikisha wanabaki madarakani kwa njia haramu.
kwa hiyo tanzania hatuna wataalamu? kama tunao kwa nini tatizo hili na mengineyo yapo? na kama wazo langu si sahihi, wewe unapendekeza nini sasa? tupe basi way foward? au tuendelee na ushabiki mpaka siku mimi na wewe tutakapoambukizwa tetanus, HIV, TB au kuumizwa vibaya? au
 
Back
Top Bottom