GE2025 Makonda: Sauti ya wananchi inasikika kwenye sanduku la kupiga kura, Tupeni kura za kutosha tupiganie maendeleo

GE2025 Makonda: Sauti ya wananchi inasikika kwenye sanduku la kupiga kura, Tupeni kura za kutosha tupiganie maendeleo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema wananchi wana wajibu na haki ya kushiriki uchaguzi utakaofanyika Oktoba 29, 2025 akibainisha kuwa sauti yao inasikika zaidi kupitia kura wanazopiga kuwachagua viongozi wanaowataka.

Akizungumza na wazee katika eneo la Shule ya Sekondari Mkonoo iliyopo Kata ya Terati, Wilaya ya Arusha l Oktoba 17, 2025, Makonda alisema idadi ya kura ndiyo inayoonesha namna wananchi wanavyohitaji maendeleo katika maeneo yao, pamoja na imani na matumaini waliyonayo kwa viongozi wao.

“Lakini pia inaweka deni kwa viongozi waliochaguliwa kwa kura nyingi kwamba tusibweteke kwasababu uchaguzi ujao zikishuka kura zetu ni tafsiri ya kutofanya vizuri kwenye jamii iliyotuchagua,” Makonda amesema.


 
Back
Top Bottom