GE2025 Makonda: Samia ni Dada wa Hayati Magufuli

GE2025 Makonda: Samia ni Dada wa Hayati Magufuli

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekamilisha na anaendelea kutekeleza miradi mbalimbali aliyoachiwa na mtangulizi wake Dk. John Magufuli ikiwamo daraja la Kigongo-Busisi ambalo ni refu zaidi Ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema wakati anaingia madarakani Rais Samia watu wengi walidhani asingeweza kukamilisha miradi lakini ndani ya miaka minne ya utawala wake mengi yamefanyika kwasababu alishiriki bega kwa bega na kuzunguka nchi nzima akimsaidia Magufuli kutatua changamoto za wananchi.

“Samia ni dada wa kanda ya ziwa, alikuw anafanya kazi bega kwa bega na kakaa yake Magufuli. Mwaka 2015 na 2020 walizunguka nchi nzima, hakuna jambo asilolijua. Kazi aliyoachiwa kwa miaka minne ni ya kutukuka sana, kuna watu hawakuamini na walisema maneno mengi kuwa miradi haitotimia,” Makonda amesema wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Wilayani Sengerema, Mkoani Mwanza.

 
Screenshot_20251007_172316.jpg
 
Back
Top Bottom