PostGE2025 Makonda: Nitaenda kumlilia Rais Samia atupe Tsh. 2 Bilioni kwa ajili ya vijana wa Online TV na Content Creators

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, ametangaza mpango wa kumuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kiasi cha hadi Shilingi bilioni mbili kwa ajili ya mikopo ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya vijana waliojiajiri kupitia vyombo vya habari vya mtandaoni na mitandao ya kijamii.

Akizungumza leo, Januari 13, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Palamagamba Kabudi, Makonda amesema lengo la mkopo huo ni kuwawezesha vijana kumiliki kamera na kompyuta za kisasa ili kutoa maudhui yenye ubora wa kimataifa yanayoitangaza Tanzania vizuri badala ya kutegemea vifaa duni.

Pamoja na uwezeshaji huo, Waziri Makonda ametangaza mkakati mpya wa kuanzisha timu maalum ndani ya wizara itakayoshughulika na mawasiliano ya lugha mbalimbali za kimataifa. Lengo ni kuhakikisha kuwa habari na matukio ya Rais Samia na Serikali yanarushwa na vyombo vikubwa vya habari duniani kwa ufanisi zaidi.

Your browser is not able to display this video.
 
Hivi hiyo hela inayopatikana kwa kumlilia tu huyo fazafaka inatoka fungu gani la budget ya nchi?
 
Upigaji
 

Wanataka kuwadhibiti kiaina.
 
Tapeli hilo, watu wa Arusha wanamuulizia Schwazinneger. Alete mrejesho wa wale wanafunzi 1,000 aliosema atawapeleka India.
 
Nahisi huyu kashindwa kusema kama Johari alivyoagizwa kumkamata Mange, ila huyu katumwa kumsafisha kupitia vyombo vya habari, na yule mkwe kusafisha scene za october
 
Hahahah. Yaani Al Jazeera, CNN na BBC wameshindwa kuripoti habari ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwa sababu haijaripotiwa na TBC kwa kiingereza au kiarabu?

Kwamba "tutawapelekea" habari CNN na BBC? Hivi ndiyo nyanja ya habari za kimataifa inavyofanya kazi?

Wanaenda tena kutapanya pesa kuwa na kitengo cha habari ndani ya wizara ya habari kwa kazi ambayo kimsingi ni ya TBC.
 
Hayo mashirika makubwa habari mbaya kwao ndio huwa habari nzuri sasa sijui atapigaje pigaje hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…