GE2025 Makonda: Mafanikio ya Bandari ni matokeo ya maamuzi makini ya Rais Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema mafanikio makubwa yanayoonekana katika sekta ya bandari nchini ni matokeo ya uongozi makini, wa kisasa na wa kisayansi chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye amefanya maamuzi ya kimkakati katika kukuza uchumi wa taifa.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika katika viwanja vya Kecha, Kinyerezi, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Makonda alisema licha ya upotoshaji uliowahi kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uwekezaji wa Serikali katika bandari, mafanikio yaliyopatikana sasa ni ushahidi tosha wa maamuzi sahihi ya Rais Samia.

Ameeleza kuwa bandari ya Dar es Salaam ambayo awali ilikuwa na uwezo wa kushughulikia tani milioni 18 kwa mwaka, sasa ina uwezo wa kufikia tani milioni 27. Wakati huohuo, bandari ya Mtwara imeongezeka kutoka tani 590,000 hadi tani milioni 2.5, na bandari ya Tanga imeongezeka kutoka tani 809,000 hadi tani milioni 1.3.

“Dkt. Samia ameangalia ni wapi akiwekeza atapata matokeo ya haraka. Ndiyo maana akaamua kuimarisha lango kuu la uchumi kupitia bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga,” alisema Makonda.

Kwa upande wa mapato, Makonda alisema Serikali imeongeza makusanyo kutoka shilingi bilioni 800 kwa mwaka hadi shilingi trilioni 2, ongezeko ambalo limeiwezesha kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za kijamii.

Your browser is not able to display this video.
 
Maisha ya DAUDI ALBERT BASHITE yamejaa unafiki wa kiwango cha juu sana. Huyu jamaa anafaa kabisa kutambulika kama rais wa wanafiki wote duniani.
 

Lile la uchumi wa kati kumbe ni mwendo wa kimya kimya hadi waseme kina Paskali ..?
 
Mwenye data za bandari before and after DPWorld take over atuwekee hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…