Mgombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini Paul Christian Makonda amewataka wanaohamasisha uchaguzi
uahairishwe kwaajili ya kupisha marekebisho ya katiba wajitokeze kufanya mdahalo nae.
Makonda amesema
" Kama kuna watu wanajiamini kwamba wanazo hoja za nguvu juu ya mambo ya katiba tufanye mdahalo nao, tunawaacha watu waovu wamesema kwa nguvu nyingi mpaka ikafika hatua wakaonekana wao wapo sahihi yaani wewe unayesimamia katiba, sheria unaonekana wewe ndio mbaya wanaovunja sheria na katiba wao wanaonekana wazuri. Paul makonda Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM leo Oktoba 11, 2025 mkoani Shinyanga.