Makonda atangaza vita na watumishi hewa mkoani Dar

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

Akizungumza leo na waandishi habari, Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamalize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha (Pay Row).

Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene ni ndogo katika jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.
 
Safi sana mkuu wa mkoa, tunakuunga mkono wabane kikamilifu ili hela itakayookolewa ikasaidie mambo mengine
 
kama mkurugenzi mwenyew ni KEBWE unategemea nini kwenye huo mkoa kama si madili tu
 
..taarifa za watumishi wa serikali na mishahara yao zinapaswa kuwekwa wazi.

..Hilo lingefanyika lingepunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la watumishi hewa.

..USIRI ktk taarifa za watumishi wa umma ndiyo unaowezesha hujuma hii ya watumishi hewa.
 
Aiseeee. Jamaa ana kasi ya ajabu

Unfortunately, Magufuli ameaminishwa kuwa huyu Makonda ni mfanyakazi ili hali ni mtu wa kupenda sifa na mkurupukaji ambae ataharibu sifa ya utendaji ya Magufuli. Nitatoa mfano mmoja tu wa yule aliyekuwa mkurugenzi wa Kinondoni ambaye Makonda alimshitaki kwa ubadhilifu na kurudishwa kutoka Babati kuja kuhojiwa; ikagundulika kuwa Makonda kwa kutaka sifa alikurupuka na mashitaka ya kufikirika na yule bwana akaonekana hana hatia!!!! Magufuli should be careful na Makoda atamuingiza choo cha kike!!
 
Duh sasa ndo maana watu wanatoa taarifa kwa kukurupuka sasa alitoa idadi ya nini kama alikuwa hana uhakika no?
 
Nafsi kamwe haitaniuma elimu yangu ya form four tena ya kuungaunga. Nafarijika sana nikisoma posti kama hiz.

Ngoja nirecharge my battery (kitu cha Arusha maamae) Iniboost my energy carrying boxes here
 
Unfortunately, Magufuli ameaminishwa kuwa huyu Makonda ni mfanyakazi ili hali ni mtu wa kupenda sifa na mkurupukaji ambae ataharibu sifa ya utendaji ya Magufuli. Nitatoa mfano mmoja tu wa yule aliyekuwa mpurugenzi wa Kinondoni ambaye Makonda alimshitaki kwa ubadhilifu na kurudishwa kutoka Babati kuja kuhojiwa; ikagundulika kuwa Makonda kwa kutaka sifa alikurupuka na mashitaka ya kufikirika na yule bwana akaonekana hana hatia!!!! Magufuli should be careful na Makoda atamuingiza choo cha kike!!
We hufai kabisa. Nchi ilikuwa imeoza watu wanajitahdi kuweka mambo sawa we unaleta mambo ya kjinga
 
Kaza buti Dar ndio wanako patikana wajaja wengi
Haiwezekani kuwepo na 79 tu
 
Back
Top Bottom