Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,034
- 7,590
Tunajua alivyowapoteza wapinzani dar mpaka sahivi hawana hari. Hii nguvu na udhubutu wa huyu kijana inaonekana sasa kuwa tishio jipya dhidi ya vijana wenzie wenye ndoto za juu katika chama chake.
Ubunifu wake, uwezo wake mkubwa, ukada wake tokea uvccm na kuzidi kujijenga kisiasa; haya mambo yameanza kuzisumbua fikra na harakati za wenzie chamani na serikalini. Kuna wanaoona ujio wa kijana huyu kama mwisho wa ndoto zao, nafasi zao na vyeo vyao. Wanatamani hili lidhibitiwe na kukoma haraka, wanaombea huyu kijana apate ajari kubwa ya kisiasa. Wako vijana wengi wenye rika lake ambao ni wabunge, mawaziri na viongozi serikalini wanaojiona tayari wanaenda kupotea.
Hili genge limeamua kuungana na wapinzani bungeni kuhakikisha wanapambana na kijana huyu, wanajiapiza kulinda nafasi na ndoto zao kisiasa. Makonda kaonekana tishio ndani na nje ya chama, anawindwa kwa mengi, anawindwa na wengi.
Ama apande awashushe ama wapande wao na wamshushe. Ama tunapata sote ama tunakosa sote, tuendelee kutega masikio. Yetu macho.