Nibozali
JF-Expert Member
- Oct 15, 2016
- 572
- 1,055
Kuna wanashindwa kutofautisha hivi vitu viwili na badala yake wameungana na Makonda anayejifariji kuwa anashambuliwa kutokana na vita ya dawa za kulevya aliyoianzisha.
Mh Makonda anatumia vita ya dawa za kulevya kama mwavuli Wa kujificha na kukwepa kujibu/kuwajibika juu ya tuhuma za kununua vyeti zinazomkabili.
Mara kadha amenukuliwa akidai kuwa vita yake dhidi ya madawa ya kulevya imefanya aandamwe na watu kwa kuzushiwa tuhuma mbalimbali. Huenda kuna ukweli katika maneno yake ingawa sitakubaliana naye kama hatofanya yafuatayo
1. Kutoka na vyeti halisi na kuuthibitishia umma kuwa yeye alianza shule ya msingi akiitwa Paul, akaenda secondary na kumaliza akiitwa Paul na hatimaye chuo/vyuo aliposoma na kumalza akiitwa Paul. Pia kama kuna mabadiliko ya majina yalifanyika aeleze yalifanyika akiwa katika hatua gani ya elimu?
Sipingani na kazi anayoifanya lakini pia sikubaliani na yeye kujificha kwenye mwavuli Wa dawa ili kukwepa tuhuma za kughushi vyeti katika elimu yake zinazomkabili
Ni ufinyu Wa fikira kuchanganya vitu hivi viwili, kinachotakiwa ni Makonda kujibu tuhuma zinazomkabili, au mamlaka husika kuzifanyia kazi tuhuma hizi huku vita dhidi ya dawa za kulevya ikiendelea kama kawaida.