Makinika! Sio kila changu ni binadamu

Makinika! Sio kila changu ni binadamu

Kuna simulizi ya kweli ya jamaa mmoja nilisikia Clouds kwenye PB,jamaa alipanda Daladala ,kwenye siti akakaa karibu na demu mmoja mzuri sana kavaa hijabu,Jamaa akasema uzalendo ukamshinda akamuuliza jina akatajiwa wakaendelea na stori demu alipofika kwenye kituo akataka kushuka jamaa akamuomba namba ya simu ila demu hakumpa akamwambia tutakutana tu

Anasema zimepita kama simu mbili hivi anaona simu ngeni inaingia,kupokea anauliza nani demu akasema ni mimi Fulani tulikutana kwenye daladala,Jamaa akashangaa sana akauliza namba zangu umepata wapi?demu akasema we potezea tu,basi jamaa hakujali sana maana demu alikuwa amemchanganya.

Jamaa akaanzisha uhusiano na demu ila alimpa masharti kadhaa,nadhani baadae alihisi huyu demu sio wa kawaida sasa akawa anataka awasimulie washikaji basi kila akikaa na washkaji alitaka tu kuanza kusimulia demu anapiga simu hapo hapo anamwambia najua unachotaka kuwaambia na ukisema utajuta kwa kitakachokupata.
Jamaa anasema alihangaika sana na hio hali sikumbuki mwisho ilikuwaje ila kwa ulichokisema Mshana naamini kabisa kuna watu tunakutana nao barabarani, kwenye mabasi,masokoni nk lakini sio binadamu kwahio tuwe makini sana.
 
Na ndio maana huwa nawasihi sana wale wanaotaka kuona wachawi live waachane na hiyo habari maana hawataona wachawi tuu wataona kila kitu kisichoonekana kwa macho ya nyama na ndio mwanzo wa uchizi
 
Ni Ukweli usiopingika 100%
Kwanza mkuu Mshana Jr nikushukuru na kukupongeza kwa kutuzindua ufahamu juu ya jambo hili.
Mada zako huwa zinatuelimisha sana mkuu. Hivi Kuna watu humu wanachukulia mzaha jambo hili.

Mimi binafsi ni mpenzi sana wa kujifunza na kufatilia mada na masomo mbalimbali ya kiroho (spiritual)
Ni Ukweli usiopingika kuwa Tendo la ndoa ni AGANO. Mnapokutana mwanaume na mwanamke pale kwenye Tendo maana yake mnafanya AGANO mbali na kuuburudisha mwili, kwenye ulimwengu wa roho kuna vitu mnabadilishana, ikiwemo laana, mapepo, mikosi, mabalaa, nuksi baraka~(hiyo huwa nadra sana)
Ndio maana kuna mwanamke/mwanaume ukilala nae then ukaenda kwenye mipango yako inaharibika yoote, iwe kazi, biashara, interview, n.k kwa wale wanaofanya bishara nadhani wameelewa ninachomaanisha.
Ki Ukweli jamii sasa hivi ipo kwenye hari mbaya sana hususani kwenye masuala haya ya kiroho. Ni wachache sana tuliojitambua.

Guys, unapojamiiana na Mwanaume/mwanamke tambua kua umebeba laana kuanzia ya Bibi yake+ ya babu yake+ ya mama yake+ ya baba yake+ laana yake mwenyewe. Sikwambii kwenye mapepo,, sikwambii kwenye nyota inavyo chafuka (kismat).
Jiulize umelala na wangapi? Umebeba laana ngapi?
Umebeba ma-roho (mapepo) mangapi aliyokuachia?
Badilika sasa

Hao wanaojiuza wenyewe kutwa wanabadilisha waganga wakuwatengenezea makafara ya kuwavutia wateja wao, na mazindiko yenye maagano mbalimbali.
Mbegu zako unazommwagia zinathamani sana kwà mganga wake, siku utakayogeuzwa kizimba ndo utajua hujui. Haya mambo yapo usifikiri utani.
Ndio maana watu wengi utawaona wanakimbilia sana kwa waganga wakidai mambo yao yameharibika ghafla, wengine wanadai eti wamerogwa kumbe tabia zao ndo zimewaroga.
Unalala na mtu hata humjui anapotoka, asili yake, ukoo wake, nyota yake. Kisa tamaa za mwili zimekutawala. Nakuombea Mungu akusaidie sana

Mungu alipo kataza zinaa hakua na maana kua anauonea donge mzigo wako hapana.
Zinaa mbaya jamani, itakuadhibu kimwili then ikumalizie kiroho.

Ushauri wangu kwa vijana na jamii kwa ujumla, tutulie kwenye ndoa zetu kama umeoa, kama bado hujaoa basi vuta subra mpaka utakapojaaliwa kuwa na mwenza sahihi.

Mungu akusaidie Sana Ufahamu
Dah kwa hali hii turud tu CHAPUTA
 
Aisee ni kama kila kona tunawindwa kuna kipindi nikiwa uchumi wa kati , niliajiri mwanamke mmoja kunisaidia kufua baadhi ya nguo na usafi wa ndani, alikuwa kama anajilengesha halafu mimi sina mpango kuna siku aliniletea chakula 🍗🍟🍚🍛 sijui kilibaki walikuwa na sherehe kukila ndio ikawa kosa sijui kilikuwa na nini ila alinimiliki karibia mwaka mmoja na nusu.

Mwanzoni alikuwa hata hanivutii ila ilikuwa nikimuona kama nachanganyikiwa najiona nipo juu ya dunia mshahara wake ulikuwa 30,000 kwa mwezi maana alikuwa anakuja na kuondoka, ila alifikia hatua akiomba hata 300,000 siku hiyo nitazunguka kama ni kukopa lazima azipate, alinipa raha yule mwamamke ila uchumi uliyumba na nilikuwa sipingi mawazo yake. Naiskia ana duka la jumla siku hizi Tabata na mimi ndio kama naanza kujitafuta upya maana mikosi na uzembe viliniandama, sasa hivi naishi kwa akili sana na hawa viumbe...hata shuleni tulifundishwa kisa cha "ngoswe penzi kitovu cha Uzembe" 🙉
 
Back
Top Bottom