Makinda tushike neno lipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda tushike neno lipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Feb 9, 2011.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh Makinda. Mimi ni miongoni mwa watu waliokupongeza sana ulipochaguliwa. Sio kwa sababu nilidhani kuwa unamzidi Sita, bali kwa sababu niliona wewe nawe unaweza ukipewa nafasi. Sikuamini waliosema umetumwa na bado sijaamini.

  Ila kuna haja ya kuangalia kwa haraka impression utakayoitengeneza hapa mwanzoni.
  Kwa kuwa suala la kambi ya upinzani ulishalisemea na kuandikwa sana na magazeti ungeonyesha kusimamia maneno yako ili kutengeneza picha ya msimamo wa maneno yako hapa mwanzoni.
  Sidhani kama itakuwa ni jambo jema kwa mtu wa hadhi kubwa kama yako watu waanze kupuuza maneno yako kwa kuwa hawajui kama hutabadilika.
  Kwa kuwa kipindi hiki ni cha tofauti sana na wakati uliopita, watu wengi wanajua haki iko wapi hata kama watu hao ni watoto wetu. Kwa ushauri wangu ni kuwa NI VEMA UKAANZA KUTENGENEZA MISIMAMO ILI KUITHIBITISHIA JAMII AMBAO NDIO WAAJIRI WETU KUJISIKIA KUWA WANAYE MTU SAHIHI.
  Kama picha kama hii itaendelea kwa viongozi wetu tunaowaheshimu kutokusimama na maneno yao basi Imani yetu itaondoka.

  Kama maslahi ya taifa ndiyo yaliyo juu, chama makini kinahitaji kusimamia kamati za bunge zilizo nyeti kwa maslahi ya watanzania. Kama serikali na chama tawala wanataka kusimamia uadilifu basi hawana la kuogopa wala kuficha.

  Watapenda wakaguliwe na hata wakosolewe. Timu inayodhaniwa kuwa kubwa inapoanza kuogopa timu wanaocheza kwa soksi kwa kuwa hawana hata mpira, basi kila mtu atajiuliza maswali au ataanza kupuuza timu hiyo.
   
Loading...