Makinda, Ndugai wageukwa

Makinda, Ndugai wageukwa

Out of wote waliosoma na kuchangia mpaka sasa, peke yako ndo hujaelewa...... We utakuta una tatizo, haiwezekani usielewe maelezo yaliyo wazi kiasi hicho..

hata me nilishangaa koment ya jamaa,halafu hii si makala ni habari
 
sasa naelewa kwanini sitta alikataa HOJA YA RICHMOND ISIJADILIWE CHINI YA MAKINDER HADI ATAKAPORUDI KWENYE ZIARA YAKE,ingawa watanzania walimzodoa na akaamua kuomba radhi lakini mwisho wa siku nimemuelewa

hata mimi sasa nimeelewa!
 
Jumanne Maghembe...Pia alisema hoja hiyo iondolewe kwa vile inazungumzia tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam wakati tatizo la maji ni la nchi nzima.
Sikujua kwamba kumbe huruhusiwi kutoa hoja kuhusu jimbo lako peke yake kama unaongelea tatizo ambalo lipo Tanzania nzima.

Kwa hiyo ukileta hoja ya kudai maelezo ya, tusema labda, kuhusu watu wamepigwa risasi na polisi Arusha serikali kwa mujibu wa kanuni za bunge itatakiwa ikwambie watu wanapigwa risasi na polisi all over the place nchini, wewe umeona kwako tu? Ondoa hoja mezani.
 
Mbaya zaid clouds wanatamani wawe wanatangaza huku wamepakatwa na mafisadi this is too much lakini mimi kwa kutumia nafasi yangu ntawashkisha adabu msipo badilika.
 
Ni ngumu sana kusimaia uongo na kukandamiza ukweli.Hawa maji sasa yanawafika shingoni na kila mtu anataka apone kivyake,wale vinara (Ma-kinda na *******) watakaobaki kama kafara.

Halafu Kuna Mtu mmoja anayeitwa Pius Msekwa akihojiwa jana, alisema hili Bunge ni la Kizazi kipya, lakini akamsifia Bi Kiroboto kuwa anaendesha Bunge vizuri kwa kufuata kanuni (ambazo nyingi aliziweka huyu GAMBA) badala ya kumshauri atumie busara kufuatana na hali halisi iliyopo sasa
 
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea na vikao vyake mjini Dodoma ambako wabunge wanajadili mambo mbalimbali ambayo yanatarajiwa kuwa na maslahi kwa watanzania na taifa kwa ujumla.
Katika mkutano huo unaoendelea huko Dodoma, wiki hii baadhi ya wabunge waliwasilisha hoja binafsi ili ziweze kujadiliwa na Bunge hilo na kutolewa maamuzi na kisha kutekelezwa na Serikali.

Miongoni mwa Wabunge waliowasilisha hoja zao binafsi ni Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala (CCM) na John Mnyika (Chadema).

Hoja ya Mbatia ilikuwa ni kutaka uboreshwaji wa elimu nchini, Dk. Kigwangalla alihitaji Bunge kuiagiza Serikali kuanzisha mfuko wa kuwawezesha vijana wanaohitimu elimu ya juu ili utumike kuwapatia mkopo kwa ajili ya kupata mtaji wa kuanzisha vitegauchumi na kuzalisha ajira, wakati hoja ya Mnyika ilitaka Serikali iwajibike katika uboreshwaji wa huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam.

Kabla ya kusonga mbele nisema kuwa hoja zote za wabunge hao, bila ya kujali itikadi za vyama vyao zilikuwa ni nzuri na zenye maslahi kwa watanzania na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, badala ya Bunge kutimiza wajibu wake wa kujadili, kuchambua na kutoa maagizo kwa Serikali, halikufanya hivyo na badala yake limegawanyika vipande vikubwa viwili vilivyotokana na itikadi za vyama vyao vya siasa! Kipande cha kwanza ambacho ni kukibwa kwa idadi ya wabunge lakini kidogo kwa uzito wa hoja ni kile kinachoundwa na wabunge wa CCM ambacho kazi yake kubwa ni kuilinda Serikali ‘isivuliwe nguo’ bungeni! Kipande kingine ambacho kinaonekana kuwa kidogo, kisichoweza kupitisha maamuzi peke yake kutokana na udogo wake kwa idadi ya wabunge, lakini kikubwa kutokana na uzito wa hoja ni kile kinachoundwa na wabunge wa kambi ya upinzani.


Vipande hivi vinapaswa kuunganishwa na kiti cha Spika ambacho kwa bahati mbaya sana na chenyewe hivi sasa hakiko imara, kinayumba na kushindwa kusimamia ipasavyo mijadala inayoendelea bungeni, hali ambayo inasababisha Bunge hilo sasa kuwa mithili ya klabu cha pombe za kienyeji! Kiti hicho cha Spika mimi nakifananisha na viatu vikubwa ambavyo amepewa mtu mwenye mguu mdogo ili avivae na sasa vinamlegea kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea vizuri! Tangu kuwepo kwa Bunge linaloundwa na wabunge wa vyama tofauti vya siasa nchini, kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimekwishakaliwa na watu watatu.

Watu hao ni Pius Msekwa aliyekuwa wa kwanza kukalia kiti hicho tangu Bunge la mfumo wa vyama vingi lilipoanza rasmi mwaka 1995, akafuata Samwel Sitta aliyekalia kiti hicho mwaka 2005 hadi 2010 kabla ya kuingia kwa Spika wa sasa, Anne Makinda. Wakati Musekwa na Sitta wakikalia kiti hicho, Naibu Spika alikuwa ni Makinda, na baada ya yeye (Makinda) kukabidhiwa kiti hicho, naye alikabidhi mikoba ya unaibu Spika kwa Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai ambaye huko nyuma aliwahi kuwa mwenyekiti wa Bunge. Kwa ufupi naweza kuelezea japo kidogo tabia za viongozi hawa walipokuwa wamekalia kiti cha Spika ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa zilitofautiana sana. Katika uongozi wa Msekwa, kiti cha Spika kilitawaliwa na ubabe ambao kutokana na wabunge wengi (hata wale wa upinzani) kuathiriwa na kanuni za bunge hilo zilizotokana au kurithiwa na mfumo wa bunge lililotangulia ambalo lilikuwa la mfumo wa chama kimoja, wabunge wote walilazimika kunywea na kutii ubabe wa kiti. Katika Bunge lililoongozwa na Sitta, aliyekuwa na kaulimbiu ya Kasi na Viwango (Standard and Speed), kulikuwa na kiwango fulani cha wabunge wote kupewa haki sawa ya kutoa ‘nyongo’ zao na hivyo kuisimamia vema Serikali hata kama usawa haukuwa wa asilimia 100 kwa vile kuna mahala alikolazimika ‘kuibeba’ serikali ya chama chake Ni katika kipindi hicho ambapo watanzania kwa mara ya kwanza walishuhudia Serikali ikiwekwa kitimoto na Bunge hadi kufikia hatua ya Serikali ‘kuanguka’ kwa Waziri Mkuu kuachia ngazi na baraza zima la Mawaziri kufumuliwa na Rais kabla ya kusukwa upya. Kwa mtazamo wangu siwezi kuwa na kigugumizi kusema kuwa Bunge lililoongozwa na Sitta linaweza kuwa ni Bunge la kwanza na la mfano wa kuigwa katika historiya ya Bunge la Tanzania.

Nasema hivyo kwa sababu pamoja na upungufu mdogo mdogo uliojitokeza, lakini Bunge hilo liliweza kuonyesha uhai kwa kuisimamia Serikali ipasavyo na hata kurejesha imani ya Bunge iliyokuwa imepotea kwa watanzania. Lakini pia jambo lingine ambalo Sitta alilifanikisha kwa ufanisi ni kuwaunganisha wabunge karibu wote ndani na nje ya Bunge, bila kujali itikadi ya vyama vyao kwani kulikuwa na Bunge moja na sio vipande ninavyoviona leo pale Dodoma.

Ni Sitta aliyeruhusu mijadala mizito kujadiliwa bungeni, hali ambayo ilisababisha Serikali kuwa katika wakati mugumu na hivyo ‘kuchangamka’ kwa kuwajibika kwa wananchi. Inasadikika kuwa ni kutokana na msimamo wa Sitta wa kutozuia hoja za msingi kujadiliwa bungeni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kinachounda Serikali kikagoma kumteua kugombea tena nafasi hiyo ya uspika kwa kisingizio kuwa ilikuwa ni zamu ya mwanamke kukalia kiti hicho!

Hapo ndipo CCM ikampitisha Anne Makinda kugombea nafasi hiyo na kutokana na wingi wa wabunge wa CCM hapakuwa na namna ya kiti hicho kwenda kwa mtu mwingine isipokuwa Makinda! Tangu Spika Makinda na naibu wake Job Ndugai wakabidhiwe rasmi kiti hicho, mambo yamekuwa yakienda ndivyo sivyo ndani ya ukumbi wa bunge.

Ladha na harufu nzuri ya mijadala ya bunge iliyokuwa imeanza kujitokeza wakati ule wa uongozi wa Spika Sitta hivi sasa imetoweka ndani ya ukumbi wa Bunge, badala yake watanzania siku hizi hawasikilizi hoja, bali wanachokisikia ni kelele za taarifa spika, uuongozo, kejeli na matusi miongoni mwa wabunge! Sina hofu na wala sitakubali kufuta kauli kwa kusema kuwa hivi sasa Bunge limepoteza mwelekeo kutokana na kuwa na uongozi mbovu kwenye kiti cha Spika! Nasema hivyo kwa sababu hivi sasa watanzania tunashuhudia hoja za msingi kabisa, tena zenye maslahi kwa watanzania na taifa kwa ujumla zikikataliwa au kupingwa kwa ushabiki wa itikadi za vyama eti kwa sababu tu zimetolewa na mbunge wa upinzani.

Wahenga walisema kuwa penye ukweli, uwongo hujitenga, naamini kuwa japo hawawezi kutamka hadharani, lakini ndani ya mioyo yao, Spika Makinda na Ndugai wanakiri kuwa jahazi lao la uongozi wa Bunge hivi sasa linakwenda mrama!

Hata nitakuwa siwatendei haki nisiposema kuwa haya yote yanatokea bungeni sio kwa utashi wao, kwani hata wao kama viongozi wangependa kuona kazi zao zinakwenda katika mpangilio mzuri na zinaleta tija kwa watanzania wote. Isipokuwa naamini kuwa inawezekana kuna nguvu nyingine iliyo nje ya utashi wao ambayo inawasukuma kufanya maamuzi yanayozingatia au kulinda maslahi ya chama chao ambayo wakati mwingine huwa siyo sahihi au hayakubaliki kwa wabunge wa upinzani na baadhi ya wabunge wa CCM na hivyo kulifanya jahazi lao ziende mrama.

Ikumbukwe kuwa Sitta alifanikiwa kuishinda nguvu hiyo, akafanya mambo yake kwa mafanikio lakini hakuweza kurejea kwenye nafasi hiyo baada ya kipindi chake cha miaka mitano kumalizika. Hivyo inawezekana Spika Makinda na Ndugai wanalitambua hilo na huwenda wanapenda waendelee kukalia kiti hicho kwa miaka mitano mingine ijayo, hivyo wanaogopa kufuata nyayo za mtangulizi wao! Nadhani kama Spika Makinda na Naibu wake, Ndugai wanahitaji kubadili mwelekeo wa bunge kutoka kwenye upepo mbaya unaovuma hivi sasa kwenda kwenye njia sahihi, kwanza wanapaswa kusahau matarajio ya kuendelea na nafasi hizo kipindi kijacho, wakaweka kando itikadi za vyama vyao vya siasa, waamue kutenda haki kwa wabunge wote na kuruhusu mijadala yenye maslahi kwa taifa hata kama inaiumziza Serikali iliyoundwa na chama chao.

Hivyo ndivyo vilikuwa viatu alivyovivaa Sitta na kuwachia na wao wavivae, lakini vimeonekana vkubwa kwao na hivyo kuwapwaya, inawezekana kwa miaka miwili iliyosalia kuhitimisha gwe yao, bado wanayo nafasi ya kuhakikisha viatu hivyo vinawatosha miguuni, nawashauri waendelee kuweka mazingira ya viatu hivyo kuwatosha miguuni!

Mungu libariki Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!


Mungu Ibariki Tanzania!.
 
Fitna zilizotumika kumtoa SPIKA SITTA ndio zinaonyesha matunda yake. Kwao ni chama kwanza, wananchi baadaye.
 
Ukishaona prof anakuwa mpiga porojo hapo kuna nini???watakumbukwa kwa kuweka historia ya ukandamizi ....wanasema mtaji wao ni vijijini saizi kila sehemu ni mabadiliko kazi ipo kikwete ni raisi wa mwisho toka ccm
asubuhi nimemsikiliza mchambuzi mmoja itv akiongelea suala hilo, hakika nimejisikia kukosa ujasiri wa kiume.
Kwa mujibu wa sheria ,taratibu na kanuni, waziri jukumu lake ni aidha kuongeza hoja au kupunguza baadhi ya hoja katika hoja binafsi inayowasilishwa na mbunge, na wala hana mamlaka ya kuiondoa.
Alichofanya prof. Magembe ni kuiondoa hoja ya mnyika kwa visingizio visivyo na mashiko.
 
clauds mimi siwalaumu kivile,it is true hawawezi ipinga serikali,ila wanachofanya ni kujaribu kuwa goodridence,wanaojua tafsiri yake watanisaidia
 
• Wabunge, wadau wa siasa waanza kukumbuka Bunge la Samwel Sitta


na Mwandishi wetu




UBABE unaolalamikiwa na wabunge wa upinzani dhidi ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, umeendelea kupingwa kila kona, huku waziri mwandamizi katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, naye amejitokeza kupinga namna shughuli za Bunge zinavyoendeshwa.

Baadhi ya wabunge waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamefikia hatua ya kusema kuwa kwa hiki kinachotokea sasa, Makinda na Ndugai wameshusha heshima na hadhi ya Bunge iliyoachwa na Samwel Sitta, aliyejulikana kama Spika wa Kasi na Viwango.

Baadhi ya akina mama wamefikia mahali pa kusema kuwa rekodi mbaya inayowekwa na Makinda bungeni inawaharibia wanawake, hasa wale waliokuwa wanawaza kuwania nafasi za uongozi wa juu, na waliodhani mama huyu angeweza kuwa mfano mwema wa akina mama katika uongozi.

Sambamba na waziri huyo, pia Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amedai wabunge wa CHADEMA hawatumwi na Katibu Mkuu wao, Dk. Willibrod Slaa kufanya vurugu bungeni bali wanatetea haki zao.

Kwa upande wao, baadhi ya wabunge wa CCM waliokataa kutajwa, wamewalalamikia Makinda na Ndugai kuwa uendeshaji wao wa shughuli za Bunge, unawapa sifa wapinzani.

Makada hao wa CCM walisema kuwa hoja binafsi mbili zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani na kisha kuondolewa katika mazingira ya kutatanisha, zimewapa sifa zaidi wapinzani.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini Dodoma, waziri huyo mwandamizi aliyeomba kuhifadhiwa jina lake, alisema kuwa haungi mkono kiti cha spika kuondoa hoja hizo kwa sababu zozote zile.

"Hoja ya Mnyika ilihusu tatizo la maji jijini Dar es Salaam. Ni tatizo kubwa sana na kila mkazi wa jiji hilo anajua. Ukiiondoa kwa sababu za kukiuka kanuni, mwananchi ambaye hajui kanuni hatakuelewa.

"Mwananchi anajua Mnyika katoa hoja nzito kumaliza tatizo la maji, wabunge wa CCM wamekataa. Haya mengine ya kanuni sijui hoja gani ijadiliwe kwanza, mwananchi haelewi," alisema waziri huyo.

Waziri huyo ambaye ni maarufu kutokana na msimamo wake katika nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika, alisema kuondolewa kwa hoja ya Mnyika kuhusu tatizo la maji Dar es Salaam, kumewaweka pabaya sana wabunge wa CCM wa mkoa huo.

Alisema ili CCM ibaki salama na ishinde majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2015, lazima serikali ihakikishe inatekeleza ahadi iliyotoa bungeni wakati wa kujibu hoja ya Mnyika, kwamba ifikapo mwaka 2015, tatizo la maji litakuwa historia katika jiji hilo.

Alipendekeza kuwa ili kiti cha spika kiendeshe mijadala ya hoja binafsi zenye kugusa moja kwa moja matatizo ya wananchi, ni bora akakaa na watoa hoja hata zaidi ya mara tatu kujadiliana nao ili inapokuja bungeni isikwamishwe na kanuni.

Alitahadharisha kuwa wapinzani ni wajanja, kwani hoja wanazoibua zinagusa matatizo halisi ya wananchi, na wabunge wa CCM wanapopingana nao, hawawezi kueleweka.

Kauli ya waziri huyo inaelekeana na ile ya Dk. Slaa aliyoitoa juzi, akidai kuwa kiti cha spika chini ya Makinda kimepwaya kwa maamuzi tofauti na ya wakati ule wa Bunge la Tisa chini ya Spika Samuel Sitta.

"Mimi nasema afadhali ya Sitta mara kumi kuliko huyu Makinda. Sitta alikuwa na aibu ya kupindisha sheria, na ilikuwa ukimbana kwenye hoja anakubaliana na hoja yako kwa manufaa ya Watanzania," alisema Dk. Slaa.

Naye mmoja wa wabunge wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, alisema kuondolewa kwa hoja ya Mnyika ni kitanzi kwao.

"Kwenye kikao cha ndani, CCM tulishapanga kukwamisha na kuiondoa hoja ya Mnyika. Lakini kama ingefika hatua ya kuchangiwa, ningechangia kwa ukali zaidi kuishambulia serikali itimize ahadi yake," alisema bila kutaka kutajwa.
Wiki iliyopita, Mbunge wa Ubungo, Mnyika na wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), waliwasilisha hoja binafsi, lakini ziliondolewa.

Mbunge mwingine wa upinzani aliyeleta hoja binafsi ni James Mbatia (NCCR Mageuzi).

Mbatia aliye mbunge wa kuteuliwa na rais, alileta hoja nzito ya udhaifu wa elimu nchini ambayo ilizua mjadala mkubwa.

Hoja ya Mbatia iliyozua mjadala mkubwa bungeni, ilipingwa na wabunge wote wa CCM na baadaye Naibu Spika, Ndugai aliipitisha kibabe huku wabunge wote wa kambi rasmi ya upinzani wakisusia na kutoka nje.
Hoja ya Mnyika ambayo ilihusu uboreshaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam, iliondolewa baada ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe kuja na hoja ya kutaka iondolewe kwa madai kuwa tayari serikali imetenga sh trilioni 1.8 kwa ajili ya kuboresha huduma na miundombinu ya maji.

Pia alisema hoja hiyo iondolewe kwa vile inazungumzia tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam wakati tatizo la maji ni la nchi nzima.

Hata hivyo, Mnyika tayari alishafanyia marekebisho hoja yake kwa kuingiza utekelezaji wa miradi ya maji nchi nzima.

Alipanua wigo wa hoja yake kwa kuingiza masuala muhimu kuhusu Programu ya Maji Safi na Mazingira Vijijini (RWSSP), maarufu kama Mradi wa Vijiji Kumi ambao unatekelezwa katika halmashauri za Dar es salaam na wilaya zote nchini.

Nassari alileta hoja kuhusu matatizo yanayolikabili Baraza la Mitihani nchini (NECTA) na kupendekeza marekebisho yake.

Hata hivyo, hoja hiyo iliondolewa kwa kile Spika Makinda alichosema kuwa kukithiri kwa vitendo vya utovu wa nidhamu kwa wabunge wakati wa kujadili hoja hizo binafsi.


Lipumba anena

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa hakuwatuma wabunge wake kufanya vurugu bungeni bali wanafanya hivyo kudai haki zao.

Kauli ya Lipumba inakuja huku kukiwa na upotoshaji unaoenezwa kuwa Dk. Slaa ndiye anachochea vurugu hizo kwa wabunge wake.

Badala yake mwanasiasa huyo alifafanua kuwa wabunge hao walikuwa na haki na kujenga hoja katika madai yao ya msingi, hasa kwa kuwakilisha matatizo ya wananchi wao.

Akizungumza jana na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya Mahakama Kuu, Prof. Lipumba alisema kuwa kupindisha hoja binafsi ya Mnyika si haki na maadili ya kiti chao.

Lipumba alisema kuwa kuwapinga wabunge hao na kuziondoa hoja zote binafsi wanazowakilisha kwa ajili ya matatizo ya wananchi si haki, na inaonesha upungufu katika kiti hicho hasa katika kutenda haki.

"Inasikitisha spika na naibu wake hawafuati utaratibu ndiyo maana sisi CUF tumependekeza katika katiba mpya spika asiwe mbunge," alisema.

Siku mbili zilizopita, Bunge lililazimika kuahirisha vikao kabla ya muda wake kutokana na kutoelewana kwa wabunge wa upinzani, kiti cha spika na serikali kwa upande mwingine, wakati wa kujadili na kupitisha hoja binafsi za wabunge.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, alisema kuwa inasikitisha Bunge kuwa na hali hiyo wakati hoja binafsi inatakiwa iheshimiwe.

Alisema kuwa kuzuia hoja binafsi ya mbunge si jambo jema na kumtaka Naibu Spika, Ndugai kutumia hekima badala ya msuli.

"Kutumia msuli haifai, na kinachoonekana dhahiri alipania kufifisha hoja ya upinzani. Kiti cha spika kinataka mtu mwenye busara na hekima, yaani imeonekana kuwa kiti hicho kinakwamisha hoja za upinzani," alisema.
Ninamkumbuka SS speed and standard Samuel Sita. Wakati anabanwa na magamba wenzie kuwa anakififisha CHAMA kwa kuwapa wapinzani nafasi!! Alijibu kama sera ya chama chetu ni UFISADI tuseme!. Sasa wamewapata makuwadi wa UFISADI kuongoza mafisadi. NDUGU _GAY na Ma-Kinda ya mafisadi.
 
tunawashauri wapumnzike kwa manufaa ya umma maana wanawapa wapinzani mtaji kuelekea 2015
 
safi SP kwa maelezo makini wao wanang'ang'ania analogia wakati huu ni wa digital wasipobadilika miaka miwili iliyobaki itakuwa migumu sana kwao wanaweza kuiona kama karne mbili.
 
Hata wapinzani wakiwaambia wabunge wa CCm wanatia aibu kwa kutovaa nguo wao watawaambia kuwa nguo zao ni za kitani.

Wananchi wa DSM wameelewa kwamba CCM haiko hapo kwa ajili yao bali kwa ajili ya ufisadi na rushwa.
 
Samweli Sitta tutamkumbuka daima bila yeye Richimond.EPA.MEREMETA,DOWANS. Tusingejuaga kamwe lakini kutokana uchungu wake na nchi alikubali hoja hizo kujadiliwa.na hatimae waziri mkuu kujiuuzulu.
 
Source Gazeti la Vitumbua(Tanzania Daima).Chadema mnahangaika sana
 
Halafu Kuna Mtu mmoja anayeitwa Pius Msekwa akihojiwa jana, alisema hili Bunge ni la Kizazi kipya, lakini akamsifia Bi Kiroboto kuwa anaendesha Bunge vizuri kwa kufuata kanuni (ambazo nyingi aliziweka huyu GAMBA) badala ya kumshauri atumie busara kufuatana na hali halisi iliyopo sasa
Bado watajigawa wao wenyewe kwa madhaifu yao,ushauri wa mjinga ni ujinga.Hata wazee hufikia wakati wanakuwa kama watoto(Msekwa) kushabikia ujinga.
 
Tumeishtukia pia clouds redio inatumiwa na wana CCM kwani ukisikiliza mesagi zao nyingi utaona wanakandya wabunge wa upinzani kuguna bungeni na kutoka nje. Tunajiuliza ni mwananchi gani asiyejua kuwa serikali ilioko madarakani imeshindwa kutekeleza ahadi zake.

My take, tutaacha kuisikiliza clouds kama hawatamwondoa kibonde na wale wengine wenye njaa wanaotumiwa na CCM.

usipoteze muda wako kusikiliza radio ya wahuni CLOUDS. Wanajipendekeza wapate ukuu wa wilaya.
 
Back
Top Bottom