Makinda awashukia viti maalumu

Makinda awashukia viti maalumu

king kan

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Posts
1,642
Reaction score
2,081
Spika wa Bunge, Anne Makinda ametoa ushauri wa bure kwa wabunge wa Viti Maalumu na kusema kwamba, badala ya kuendelea kubweteka katika nafasi hizo, wajinasue sasa na kwenda kugombea majimboni kwani nafasi hizo zinawapotezea heshima mbele ya jamii.

Spika anasema wabunge wa Viti Maalumu wanaonekana kuringa na kujisahau kabisa kwenda majimboni, huku akionya kwamba kitendo cha kuendelea kubweteka kitakuwa kimewaangusha wanawake wa Tanzania, ambao alisema wanategemea ushiriki wao katika chombo hicho muhimu cha kufanya maamuzi. Kwa tafsiri yoyote ile, hayo ni maneno makali ambayo pengine yatakuwa yameudhi baadhi ya wabunge hao kwa madai ya kudhalilishwa.

Source; Mwananchi
 
As speaker wa Bunge la Tanzania, tamko hilo linaonesha wazi kabisa kwamba hakubaliani na utaratibu wa viti maalum na ingekua ni madaraka yake viti hivyo vingeondolewa ili kila mbunge agombee nafasi yake. I hope she made it clear that she was talking on her own behalf and not as per official position.
Amefanya vizuri kuji-express ila sidhani kama ametumia njia inayo faa. Njia alio tumia inawadhalilisha wabunge wenzie hao.
 
Mimi naona ni kupigia mbuzi gitaa. Viti hivyo vifutwe tu.
 
Basi wakuu tuwekeni kwenye maoni yetu kuhusu katiba mpya, mi tayari nilishagaliweka hili
 
Katiba mpya ndo suluhisho

Vifutwe...Sioni maana ya viti maalum. Imagine tunapokuwa darasani jinsia zote mbili wanawake wana shika nafasi za juu. Kuna ma-daktari bingwa, waandisi, wahasibu, wanasheria na wananzuoni wanawake waliobobea...iwe vipi kwenye siasa TU NDIPO wanapata upendeleo ? Futa mzigo kwa mpiga kura...cheki Mh Mdee she did it in men dominated constituency..others may do the same
 
Makinda mwenyewe ni mzigo bungeni. Kazi kukurupuka. Wakati hizo nafasi zikiwekwa yeye ni mmoja wa wale waliosema dioooooyoooo
 
huo ndo ukweli wajtafutie wenyewe majmbo yakuwakilisha wasiwe kama kuku wa kisasa
 
ha,ha,haa. Ngoja waje vitu maalumu wenyewe watoe tamko. Chezea chakula ya wakubwa weye!
 
As speaker wa Bunge la Tanzania, tamko hilo linaonesha wazi kabisa kwamba hakubaliani na utaratibu wa viti maalum na ingekua ni madaraka yake viti hivyo vingeondolewa ili kila mbunge agombee nafasi yake. I hope she made it clear that she was talking on her own behalf and not as per official position.
Amefanya vizuri kuji-express ila sidhani kama ametumia njia inayo faa. Njia alio tumia inawadhalilisha wabunge wenzie hao.

Amekosea.

Ingawa naunga mkono alichokisema, lakini ukiwa Speaker huwezi kusema kitu kuhusu views zako personal kuhusu ubunge na utegemee zitegemewe kutenganishwa na your official capacity.

Ameonyesha kwamba kuna wabunge wa madaraja tofauti, na hawa wa viti maalum hawana hadhi kama wale wa kuchaguliwa. Kitu ambacho hakipo katika katiba wala muongozo wowote wa bunge.

Kama hayo ndiyo maoni yake alichotakiwa kufanya ni ku lobby viti hivi vifutwe, sio kuanzisha mgawanyiko bungeni na kutengeneza madaraja ya wazi kati ya wabunge.

Mara nyingine tena viongozi wa Tanzania wanaonyesha kutoelewa collective responsibility na separation of the personal from the official.
 
Spika wa Bunge, Anne Makinda ametoa ushauri wa bure kwa wabunge wa Viti Maalumu na kusema kwamba, badala ya kuendelea kubweteka katika nafasi hizo, wajinasue sasa na kwenda kugombea majimboni kwani nafasi hizo zinawapotezea heshima mbele ya jamii.

Spika anasema wabunge wa Viti Maalumu wanaonekana kuringa na kujisahau kabisa kwenda majimboni, huku akionya kwamba kitendo cha kuendelea kubweteka kitakuwa kimewaangusha wanawake wa Tanzania, ambao alisema wanategemea ushiriki wao katika chombo hicho muhimu cha kufanya maamuzi. Kwa tafsiri yoyote ile, hayo ni maneno makali ambayo pengine yatakuwa yameudhi baadhi ya wabunge hao kwa madai ya kudhalilishwa.

Source; Mwananchi

Atakuwa amesema hayo akiwa na hisia fulani hasa tuhuma kuwa kuna wabunge wa viti maalum wameupata ubunge wao kwa umahili wao wa kuvua chu..pi na wengine wakituhumiwa kuwavulisha chu..pi mabinti zao ili wao waende mjengoni.
Shame on them... hata hivyo hatutaki wabunge wa viti maalum tena maana hawajulikani wanamwakilisha nani..
 
Hawa si ndo wale wasema "NDIYOOOOOOO", na YEYE si ndo yule "NADHANI WALIOSEMA NDIYO WAMESHINDA".
Birds of the same feathers flock together
 
Spika wa Bunge, Anne Makinda ametoa ushauri wa bure kwa wabunge wa Viti Maalumu na kusema kwamba, badala ya kuendelea kubweteka katika nafasi hizo, wajinasue sasa na kwenda kugombea majimboni kwani nafasi hizo zinawapotezea heshima mbele ya jamii.

Spika anasema wabunge wa Viti Maalumu wanaonekana kuringa na kujisahau kabisa kwenda majimboni, huku akionya kwamba kitendo cha kuendelea kubweteka kitakuwa kimewaangusha wanawake wa Tanzania, ambao alisema wanategemea ushiriki wao katika chombo hicho muhimu cha kufanya maamuzi. Kwa tafsiri yoyote ile, hayo ni maneno makali ambayo pengine yatakuwa yameudhi baadhi ya wabunge hao kwa madai ya kudhalilishwa.

Source; Mwananchi

Lengo la viti maalum lilikuwa ni zuri. Kwamba wanawake wa kada zote wawakilishwe. Lakin matokeo yamekuwa tofauti kwani walioshikilia wanawakilisha kada ya aina moja tu hasa mafisadi. Angalia mifano ya Mama Sita, kuna haja gani wote wawili kuwa bungeni, huu ni ufisadi pia, angalia Sophia Simba, n.k.

Hivi viti kwa sas havihitajiki tena kwani ni mzigo kwa wananchi. Pia ni vema hata wabunge wa majimbo wapunguzwe. Tunaweza tukawa na mbunge mmoja kila wilaya.
 
neno KURINGA nimelitafsiri kama NYODO ZA KIKE.. Makinda hawezi kujenga hoja kwa kusema wenzie wanaringa sio hoja nzuri kisiasa
 
Viti maalum vifutwe tu hawana lolote kwanza sura ni zilezile miaka nenda rudi,au ni wa*****zi wa viti rasmi?
 
Sasa kitu maalum kama Vick kamata ana ubavu gani wa kujiatafutia jimbo?
 
Spika wa Bunge, Anne Makinda ametoa ushauri wa bure kwa wabunge wa Viti Maalumu na kusema kwamba, badala ya kuendelea kubweteka katika nafasi hizo, wajinasue sasa na kwenda kugombea majimboni kwani nafasi hizo zinawapotezea heshima mbele ya jamii.

Spika anasema wabunge wa Viti Maalumu wanaonekana kuringa na kujisahau kabisa kwenda majimboni, huku akionya kwamba kitendo cha kuendelea kubweteka kitakuwa kimewaangusha wanawake wa Tanzania, ambao alisema wanategemea ushiriki wao katika chombo hicho muhimu cha kufanya maamuzi. Kwa tafsiri yoyote ile, hayo ni maneno makali ambayo pengine yatakuwa yameudhi baadhi ya wabunge hao kwa madai ya kudhalilishwa.

Source; Mwananchi

Ukitaka kuwaudhi viti maalum hasa wale wa CCM, basi ongea maneno kama haya ya Makinda. Pale wameshajenga kambi yao ya kuingia kiulaini halafu wewe uwaambie waende majimboni au uweke ukomo??? watakutoa mbio wale wamama
 
Back
Top Bottom