Makinda amuumbua Makongoro Mahanga

Makinda amuumbua Makongoro Mahanga

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Posts
1,334
Reaction score
990
Sikuamini nilichokiona leo asubuhi ambapo Makongoro Mahanga alitaka kurudia mchezo uleule wa Lukuvi uliosababisha akina Tundu Lissu watolewe nje.

Makongoro alikuwa analeta 'taarifa' lakini akaanza kuhutubia. Spika palepale alimkatisha kwa kumwambia 'usianze kutuhutubia'. Hii ilimfanya Makongoro akose mwelekeo kwa taarifa yake iliyolenga kuzuia baadhi ya mijadala.

Spika akampa live kwamba 'siwezi kuzuia wabunge kujadili'.

Jibu hili lilimuudhi mmoja wa mawaziri akaomba mwongozo.

Spika akakataa akisema 'hatuwezi kukalia kuongozana tu wakati wote'.

Hakika ni kama 'I can see at least some light at the end of the dark tunnel'

Kwa uelewa mdogo kila mbuge anaweza kuimudu nafasi ya ubunge kama atakuwa hana upendeleo na wala sio mchumia tumbo.
Nachokiona kwa mama Makinda sasa kesha ona aliyemuweka kitini kaachia ngazi so hakuna maslahi tena ya RA.
Kazi ipo kwa Ndugai na wenyeviti wa kamati kama Simbachawene na manumba kuruhusu kwa usawa mijadala yenye hoja katika maslahi ya Taifa hili kandamizi.

kama si changa la macho basi tuone siku za mbele.

Huu utafiti wa Wakenya utaleta mengi! Yaelekea ameanza kunusa harufu mbaya ya 1015

sikuamini nilichokiona leo asubuhi ambapo makongoro mahanga alitaka kurudia mchezo uleule wa lukuvi uliosababisha akina tundu lissu watolewe nje.

Makongoro alikuwa analeta 'taarifa' lakini akaanza kuhutubia. Spika palepale alimkatisha kwa kumwambia 'usianze kutuhutubia'. Hii ilimfanya makongoro akose mwelekeo kwa taarifa yake iliyolenga kuzuia baadhi ya mijadala.

Spika akampa live kwamba 'siwezi kuzuia wabunge kujadili'.

Jibu hili lilimuudhi mmoja wa mawaziri akaomba mwongozo.

Spika akakataa akisema 'hatuwezi kukalia kuongozana tu wakati wote'.

Hakika ni kama 'i can see at least some light at the end of the dark tunnel'

mzee bado ni mapema sana kuanza kumwamini huyu mama kwani anatumiwa kwahiyo the next day anaweza akaku disappoint big time.

Amestuka huyo. Kaona jinsi gani Job Ndungai alivyopoteza umaarufu

Sikuamini nilichokiona leo asubuhi ambapo Makongoro Mahanga alitaka kurudia mchezo uleule wa Lukuvi uliosababisha akina Tundu Lissu watolewe nje.

Makongoro alikuwa analeta 'taarifa' lakini akaanza kuhutubia. Spika palepale alimkatisha kwa kumwambia 'usianze kutuhutubia'. Hii ilimfanya Makongoro akose mwelekeo kwa taarifa yake iliyolenga kuzuia baadhi ya mijadala.

Spika akampa live kwamba 'siwezi kuzuia wabunge kujadili'.

Jibu hili lilimuudhi mmoja wa mawaziri akaomba mwongozo.

Spika akakataa akisema 'hatuwezi kukalia kuongozana tu wakati wote'.

Hakika ni kama 'I can see at least some light at the end of the dark tunnel'

acha uchochezi na ushabiki wako usiokuwa na tija! Kwani Spika kumwambia hayo ndio kumuumbua? Angeambiwa hayo Wenje ungesemaje.

Wepesi sana kuridhika na kusahau dhiki na maumivu makubwa, tuko kama mama aliyemaliza kujifungua, inakera sana
umeongea yaliyo moyoni mwangu. Tunaridhika sana wanapotupa peremende, huku wao wakila keki.

Kushtakiwa na lissu kuwa anapendelea sasa limeanza kumuingia akilini,anajitahidi kidogo kwa sasa.tumpe muda na tuendelee kumchunguza.

angalau kidogo amesoma alama za nyakati.

Sikuamini nilichokiona leo asubuhi ambapo Makongoro Mahanga alitaka kurudia mchezo uleule wa Lukuvi uliosababisha akina Tundu Lissu watolewe nje.

Makongoro alikuwa analeta 'taarifa' lakini akaanza kuhutubia. Spika palepale alimkatisha kwa kumwambia 'usianze kutuhutubia'. Hii ilimfanya Makongoro akose mwelekeo kwa taarifa yake iliyolenga kuzuia baadhi ya mijadala.

Spika akampa live kwamba 'siwezi kuzuia wabunge kujadili'.

Jibu hili lilimuudhi mmoja wa mawaziri akaomba mwongozo.

Spika akakataa akisema 'hatuwezi kukalia kuongozana tu wakati wote'.

Hakika ni kama 'I can see at least some light at the end of the dark tunnel'

Wanajifunza kutokana na makosa.

Tunaamini kuwa kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ni kosa.

Hongera mama.

Wepesi sana kuridhika na kusahau dhiki na maumivu makubwa, tuko kama mama aliyemaliza kujifungua, inakera sana

Tumekuwa taifa la watu wanaoishi kwa matumaini tukitarajia mambo mema kwa utaratibu uleule uliotufikisha kwenye hali mbaya tuliyonayo. Hatuna tofauti na fisi anayemfuata kwa nyuma mtu anayetembea akitarajia kuwa mkono mmoja utadondoka ili apate kuula.

Spika akakataa akisema 'hatuwezi kukalia kuongozana tu wakati wote

awe anawakomalia hivyo hivyo, anapokubaliana nao kutaka mwongozo kila wakati maana yake wanamwongoza hata yeye

Back
Top Bottom