Chuo Kikuu Makerere kumuenzi Mkapa kama kiongozi bora
Na Leon Bahati
"NABII hakubaliki nyumbani kwake". Ndivyo inavyojionyesha kwa rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ambaye leo atakuwa akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa na Chuo Kikuu cha Makerere.
Nyumbani, Mkapa anakabiliwa na tuhuma nzito za kufanya biashara akiwa Ikulu, kujiuzia mgodi wa Kiwira kwa bei poa akiwa na waziri wake wa zamani, Daniel Yona, lakini leo, rais huyo wa awamu ya tatu ambaye alifanya kazi kubwa ya kuinua uchumi, atatunukiwa shahada hiyo kutokana na chuo hicho kubaini kuwa alikuwa kiongozi bora na ambaye anafaa kuigwa.
Mkapa, ambaye aliongoza nchi kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 akishughulika na ukusanyaji kodi uliosaidia nchi kufutiwa madeni, na ujenzi wa miundombinu, anaonekana na chuo hicho kuwa alifanikiwa kuimarisha demokrasia hapa nchini.
Vyombo mbalimbali vya habari nchini Uganda, likiwemo gazeti la Daily Monitor, jana viliripoti kwamba vikao vya juu vya maamuzi katika uongozi wa chuo hicho maarufu Afrika Mashariki, vilijadili kwa kina na kubaini kwamba rais huyo wa zamani wa Tanzania anastahili kupewa heshima hiyo.
Msemaji wa chuo hicho, Gilbert Kadilo alisema kwamba Mkapa, ambaye alisomea shahada yake ya kwanza chuoni hapo, atatunukiwa heshima hiyo leo kwenye sherehe maalumu ambazo pia amealikwa kuwa mgeni rasmi na ataangoza harambe ya kuchangia maboresho ya chuo hicho kikongwe.
Kadilo alisema kwamba jina la Mkapa lilipatikana baada ya mchakato mrefu uliohitimishwa uliofanywa na seneti na baraza la chuo hicho.
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Mondo Kagonyera alisema kwamba Mkapa ni miongoni mwa viongozi wa Afrika, ambao walisoma chuoni hapo, akiwa amejiunga na chuo mwaka 1957 na kumaliza 1962 na kutunukiwa Shahada ya Fasihi na Lugha ya Kiingereza.
Profesa Kagonyera aliwataja viongozi wengine waliosoma kwenye chuo hicho chenye umri wa miaka 87 tangu kianzishwe kuwa ni rais wa kwanza wa Tanzania na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, rais wa Kenya, Mwai Kibaki, kiongozi wa Nigeria Hajj Shehu Shagarna na marais wanne wa zamani wa Uganda, Godfrey Binaisa, Milton Obote, Sir Edward Luwangula Muteesa II na Yusuf Lule.
Hapa nchini Mkapa anatuhumiwa kusajili kampuni ya ANBEN na kufanya biashara akiwa Ikulu, huku familia yake na Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona zikitajwa kujitwalia mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira kinyume na taratibu, kwa bei poa ya Sh70 milioni.
Rais huyo mstaafu pia amekuwa akitajwa kutumia mamlaka yake kuandika barua na kuagiza nyongeza ya mkataba wa miaka kumi kwa kampuni ya International Container Terminal (TICTS), ambayo inaendesha kitengo cha makontena kwenye Bandari ya Dar es salaam. Pamoja na tuhuma hizo zote, Mkapa amekuwa hataki kuzizungumzia, lakini hivi karibuni alisema kwenye mkutano wa mfuko wa Mkapa kuwa "hawezi kuzuia masikio ya watu kusikia, lakini anaweza kuuzuia mdomo wake kusema", kauli iliyoonyesha kuwa ataendeleza msimamo wake wa kutojibu tuhuma zinazomkabili.
Imekaaje hii!