Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Mkuu!
Hizo ndiyo za serikali DHAIFU. Si unakumbuka ile meli ya samaki wa Magufuli ilivyo oza na kuibiwa kila kitu licha ya kuwepo ulinzi wa POLICECCM wa masaa 24. Hakuna wanalo liweza zaidi ya kujikita kwenye UFISADI. Hiyo nyumba wanaiona hailipi ndiyo maana wameitelekeza Mkuu. Labda tuwaombe Wana Msumbiji waje kuikarabati ili iwe jengo la historia kwao.
Hayo si mambo ya kipao mbele kwa CCM, Kule SUA walifanya kwa vile huwa wanapata misaada hivyo ilikuwa njia ya kujikomba kupata misada sasa hao wengine hawana uwezo kutoa misaada
Serikali ya CCM kwa kujisahau hawajambo............
Ni kweli kuwa KUSINI ni yatima laini tegemea kupokea majibu rahisi sana kutoka kwa hawa watu maana huwa siamini kama wanauzalendo kivile wa kujali kule wanakotoka na wananchi wao wa hukoNatafuta uwezekano wa kumvaa Mkuchika au Membe watoe ufafanuzi kwa nini wimbi la ufunguaji vyuo vikuu nchini hauendi kwa kasi kama mikoa ya kusini wakati kuna majengo tayari kama haya ambayo yangewexa kutumika.
Ni kweli kuwa KUSINI ni yatima laini tegemea kupokea majibu rahisi sana kutoka kwa hawa watu maana huwa siamini kama wanauzalendo kivile wa kujali kule wanakotoka na wananchi wao wa huko
Kusini walitoa rais tukajua afadhari ndugu na jamaa zetu watasikika vilio vyao pamoja na kuwa na maendeleo makubwa kama ilivyo kuwa toka enzi za zamani enzi za kituo cha biashara duniani
Nikikumbuka kitabu nilicho soma kuh sehemu kuu ya biashara duniani ilikuwa uko kusini...Simanzi tupu
I am lost in between,to buy your story OR shove it back to youUkibahatika kufika huko ndipo utakapojua kwamba mkombozi ni mmisionari, la sivyo leo tungekuwa tunaongea mengine kama ilivyotokea safari moja nilipoenda ziwa Tanganyika Km kadhaa hivi kutoka Kipili. Tulikuwa na gari dogo aina ya Landrover rangi nyeupe. Hiyo barabara ilikuwa mpya tu ilitengenezwa kwa jitihada za Mbunge Itara wa wakati huo kutokea Kate, Kitosi na kisha kuishia ziwa Tangabyika. Katika kumbukumbu yao huko ni greda lililokuwa linalima barabara. Gari iliyofuata ni chakavu landrover. Ya kwetu ingawa ilikuwa short chesis hard top na nyeupe, tulikuwa na ziada ya kuwazuia wasifuate maana ilikuwa ni mara yao ya kwanza kuona kitu kama hicho na wakawa wanasema ni bado mtoto anakua. Tuliwatahadhalisha wasilisogelee mno wakati linatembeza wanaweza pata ajali wao walisema mbona lina macho linaona? (kina macho kinaona). Mbaya saidi tulipofika mahala na kusimamisha gari wakawa wanachungulia kuona kama ni la kike au kiume. Basi ni vituko duniani kuna mambo. Kuna sehemu ambacho ni bado sana. Hiyo ilikuwa Miaka ya 90.
Hapa ni moja ya majengo ambayo wapigania ukombozi barani Afrika walikuwa wakiishi akiwamo Marais Mugabe wa Zimbabwe na hayati Samora Machel wa Msumbiji kama ilivyokuwa makazi ya wapigania haki wa South Afrika pale Morogoro kilipo chuo cha Sokoine. Umbali wa km 34 toka Lindi mjini eneo lijulikanalo kama Farm 17.
Jambo la kushangaza serikali imeshindwa kubuni njia ya kuyaendeleza majengo haya na kubaki katika hali mbaya kwa kiwango hiki kwa sababu ya kuyatelekeza. Pamoja wanakijiji hapo kuamua kuanzisha shule ya sekondari lakini hali ya majengo hairidhishi, hali ni kama pichani inavyoonekana.
Gharama ya ujenzi wa majengo hayo siku ya leo ni mabilioni ya pesa, kwa nini kisianzishwe chuo kama ilivyofanyika Morogoro SUA kuyanusuri majengo na papo majengo yaweze kutunufaisha watanzania?
Bodi ya Utalii na Watu wa makumbusho waingize katika kumbukumbu za maeneo ya kuhifadhiwa kwa ajili ya Utalii wa ndani na nje.