Leo nimeshindwa kutoa pesa naona Ada imepanda kutoka 2,700/- hadi 4,135/- na tozo imepungua kutoka 2,050/- hadi 1,435/-.
Kwa hesabu za haraka jumla ya makato yalikuwa 4,750/- kwa kutoa 55,000/- sasa ni 5,570/-
Au ukiwa kijijini Njombe kuna makato tofauti?!
Me nimechoka kulalamika. Ila nasubiria kwa hamu na shauku siku CCM ikitoka madarakani na hao wahuni waliopo katika nafasi za uongozi wakiingizwa kiifungoni kutumikia adhabu zao ikiwemo kufilisiwa mali.