Makato ya CRDB yananikimbiza

Makato ya CRDB yananikimbiza

pasodz

Member
Joined
Jan 19, 2015
Posts
59
Reaction score
10
Ndugu wanajamvi!

Naumia sana na hii bank ya CRDB kila nikiweka hela account zinakaa siku kadhaa then zinakatwa vibaya mno mpaka naonea huruma hela yangu.

Et wadau ni benki gani ambayo nikiweka hela kwa ajili ya kuhifadhi hawakati?

Niambie nihamie huko.
 
ndugu wanajamvi!
naumia sana na hii bank ya crdb kila nikiweka hela ac znakaa cku kadhaa then znakatwa vibaya mno mpaka naonea huruma hela yangu et wadau ni bank gan ambayo nikiweka hela kwa ajili ya kuhfadh hawakat niambie nihamie huko
ntashkr

Kajifunze kuandika kwanza
 
Hama hiyo bank ndiyo suluhisho, acha kulalamika. Ndiyo mana kuna bank nyingi
 
Kajifunze kuandika kwanza
Mimi naona hoja yake inaeleweka hebu tujadili hoja badala ya namna ya kuandika. Ukweli makato yqa CRDB ni makubwa mno hakuna hata faida wanayotoa inayoonekana wazi. Yaani makato ni makubwa kuliko faida au riba kwa mteja. hata mimi najiandaa kuhama. Katika benki nilizotafiti nimeona EXIM wana nafuu kubwa.
 
crdb bank ilikuwaga na vibobo vya kuweka maoni, sijui ka bado vipo. Je management inawahamasishaje wateja kuvitumia visanduku hivi? Msiogope kuhabarishwa hata kama ni kulaumiwa.
Sijui ka humu jf huwa wanasoma lakini kumekuja manung'uniko mengi recently kuonesha kuwa kuna upungufu Dr. Kimei. Hili ni ombwe la uongozi, mgema ukimsifia, tembo hulitia maji.
Where else shall we run to? Ukiziweka home, majambazi, ukienda kuzichukua, risasi hapo hapo mlangoni sijui wanakonyezwa na hao hao ma teller. Huu mpango wa kuwaweka watu pale wanaketi kwenye viti wakingojea namba kuitwa nao, mhhhh sasa hao jaamaa si wanajikalia pale wakiangalia mfuko tunaoweka wanatufuata tu. Sijui, mi nawaza tu
 
Ni lazima ukatwe account maintanance charges. Ulitaka wakuhifadhie fedha bure? Ukitaka bure weka uvunguni
 
Ni lazima ukatwe account maintanance charges. Ulitaka wakuhifadhie fedha bure? Ukitaka bure weka uvunguni

hazihifadhiwi bure huwa wanazifanyia biashara na kupata riba kubwa.

Lakini kwa maoni yangu Jee Dr Kimei hajafikia tu muda wa kustaafu? Binaadamu yeyote akikaa sehemu moja kuongoza kwa muda mrefu mwisho huishiwa na mawazo mapya.
 
Hakuna Benki yenye nafuu, zote ni majanga tupu.Hata huko NMB nako ni balaa tupu.Ukiweka hela zako hata ukitaka kujua salio tu wanakata , ukitaka kuchukua pia wanakata wakati huo huo wanakutoza hela kila mwezi wanaziita za maintainance. Hela unayoweka wanawakopesha watu wengine faida inayopstikana hawakupatii- Why? Mbona zamani walikuwa wakitoa faida ? Ama kweli Benki zote hazina urafiki na MASIKINI kote Duniani.
 
mh! mi hapo cjaona kosa kama vp ungeniambia niandkaje ingesaidia pia il kesho nikosee

Wi-Fi anajifanya yeyey ndiyo anajua kuandika vizuri bila kukosea gapyeeee!!
 
Last edited by a moderator:
labda Tanzania Postal Bank yaani benki ya posta nakumbuka washkaji fulani wao salary ikiingia kwenye hizo bank zingine wanatoa na kuweka kule posta.
 
Back
Top Bottom