Makapuku Forum

1948 - Luis Felipe Scolari anazaliwa.

Ni kocha wa zamani wa Chelsea, Ureno na timu ya taifa ya Brazil.

Aliipa Brazil ubingwa wa Dunia mwaka 2002.

Aliiongoza Brazil katika michuano ya kombe la dunia iliyofanyika katika ardhi ya nyumbani na kutolewa katika Nusu fainali na Ujerumani kwa kipigo cha 7-1.
 
1960 - Andreas Brehme anazaliwa.

Ni beki wa kushoto wa zamani wa Bayern Munich, Inter Milan na timu ya taifa ya Ujerumani.

Alisifika kwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wachache waliokuwa na uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwa ufasaha.

Anakumbukwa kwa kufunga goli pekee kwa penati katika fainali ya kombe la dunia mwaka 1990 na kuipa taji Ujerumani dhidi ya Argentina ya Diego Maradona.

Penati hiyo ilipatikana dk ya 85, wachezaji wa Ujerumani wengi wao wakaogopa kupiga yeye akapiga na kuipa ubingwa nchi yake.
 
1974 - Del Piero anazaliwa.

Mchezaji wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Italy.

Moja kati ya wachezaji bora wa wakati wote Italy imewahi kuwa nayo.

Mfungaji bora wa wakati wote katika Serie A.

Ametwaa kombe la dunia mwaka 2006 akiwa na Italy iliyosheheni mastaa kama Pirlo, Totti, Luca Toni, Fabio Grosso, Materazzi, bila kumsahau Gigi Buffon.
 
 
Leo katika Historia:

If u can't beat him, join him.

Sikumuunga mkono Trump lakini ameshinda hivyo sina budi kumuunga mkono kama Rais mpya wa Marekani.

Kwa udhamini mnono wa Donald Trump a.k.a Usiyempenda kaja niwatakie jioni njema.
 
 

Kisa?
...
Vyanzo mbalimbali vya habari vinasema kuwa aliamua kuiua familia yake kutokana na umaskini aliodai umemkabili kufikia kushindwa kuihudumia familia yake.

Lakini baada ya kuiua familia yake alioa mke mwingine na kubadili jina na kwenda kuishi mji mwingine mpaka pale alipokamatwa miaka 18 baada ya kufanya mauaji yale ya kinyama.

Alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kabla ya kupotea maisha akiwa anatumikia kifungo chake.
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…