Ifikapo umri wa miaka 2 hadi 3, watoto wengi huanza:
- Kutambua jinsia yao wenyewe (ikiwa ni mvulana au msichana).
- Kutambua jinsia ya watu wengine.
- Kuonyesha tabia zinazohusiana na jinsia yao — kama kupendelea aina fulani ya vitu vya kuchezea, mavazi, au shughuli zinazohusiana na jinsia yao katika tamaduni zao.
Hii haimaanishi kuwa wanaelewa kabisa utambulisho wao kijinsia, bali huanza kuwa na hisia ya utambulisho binafsi kulingana na jinsia yao, na mara nyingi huiga tabia wanazoziona kwa watu wazima au wenzao wa jinsia moja.
Mfano:
Mvulana wa miaka 3 anaweza kusema, “Mimi ni mvulana” na kupendelea kuchezea ‘toy’ za magari au kwa msichana anaweza kusema pia nae, “Mimi ni msichana” na kupendelea kucheza na midoli n.k