Kwasasa tunafanya mazoezi kwaajili ya kutengeneza miili ya wachezaji lakini pia na kurekebisha pale palipopungua,
lakini hayo yote yanalenga safari kwaajili ya mechi ya marejeano ambayo tunategemea kwenye tarehe 20 tutasafiri kutoka hapa Tanzania kuelekea Libya.
Ukweli usiopingika Al Ahly Tripoli ni wazuri na siyo wazuri tu ila wanajua fitna, na fitna yao ni kubwa sana tofauti na mtu anaweza kufikiri, hayo tunayafahamu vizuri lakini ndomaana tumekuwa na Mwalimu ambaye pia ni mzuri.
Hakuna mtu asiyefahamu Nchi za Kiarabu zinapokuwa Katika mashindano wanapokuwa nyumbani, kwaiyo nidhamu kubwa inahitajika sana kwa timu, nidhamu ya hali ya juu.
Lakini umakini wa kupindukia maana lolote linaweza likatokea kwaiyo tahadhari zote tumezifanyia kazi maana haziji kwa miujiza zinakuja kwa kuzitengeneza na Kwa kujiandaa kwa watu mwisho zikaingia kichwani, kwaiyo kwa hizi siku tano ambazo tutakuwa hapa Dar es salaam, tutakuwa tukitengeneza akili za watu, tabia za watu, mitazamo ya watu lakini na hali halisi ya timu zenyewe tutachezaje tukiwa kule.
Ujue kule hatuendi kucheza, sisi tunaenda kulinda lakini tutafute hata goli moja tu itakuwa afadhali, tulipate mapema itakuwa basi.
Wachezaji wote wako fiti na Watanzania wategemee maendeleo kwani tumekusudia tuendelee Kwani tunataka tuvuke hii hatua na tutaivuka kwasababu, watu wanatutia moyo, watu wana imani na sisi, watu wanatuombea, watu wanatuthamini kwaiyo tunaomba sapoti yao wote katika Dua ili tuweze kusonga mbele kwani siyo sisi tu ni pamoja na Watanzania wote
- Frank Wabare, Afisa Habari Biashara United.