Makapuku Forum

...nimekuwa nikipenda muziki wa Country bila kujali mengi nyuma yake. Kama ilivyo kwa Jazz, ambayo nayo ni genre ya muziki ninayovutiwa nayo, country imekaa kiweupe zaidi lakini hey, weupe au weusi bado masikio yanasikia utamu ule ule.

Jtatu hii nimekaa najisomea zangu news na nashtushwa na habari inayotangaza kifo cha nguli wa Country, Charles Daniels au kama anavyojulikana zaidi CDB . Kwenye anga hizi alikuwa akipiga violin aka zeze la kizungu lisilo na bass kama sauti yake.

Msikilize hapa kwenye Simple Man japo wimbo uliompandisha chati zaidi ni The Devil Went Down to Georgia.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…