Makapuku Forum

Amen
 
Infuse your life with action. Don't wait for it to happen. Make it happen. Make your own future. Make your own hope. Make your own love. And whatever your beliefs, honor your creator, not by passively waiting for grace to come down from upon high, but by doing what you can to make grace happen... yourself, right now, right down here on Earth.
 
 
Muziki: Ijumaa Njema


Ninakusalimia Kapuku na kukupongeza kwa kuweza kuifikia siku na jioni ya leo. Ijumaa ni siku nzuri, wapo tunaokwenda kuswali na wengine ndo tunamalizia kazi za kuanzia Jumatatu.

Furahiday sinaga mengi, ni burudani kwa kwenda mbele, niko Shinyanga wiki hii na nimejikalisha hapa Bakulutu pub, napoza koo

 
Ni kansa ndo ilimuondoa, hadi mauti yanamkumba mwaka 1981 mwezi Mei tarehe ya leo (Mei 11, 1981) alikuwa akivuta nusu kilo ya bangi kwa wiki. Alifariki akiwa kijana tu ana kwa kuwa aliacha vitu vingi vya kukumbukwa, hajawahi kufa mioyoni na masikioni mwa wote wanaopenda kusikia nyimbo zake.

Namuongelea mwanamuziki na miongoni mwa watu maarufu duniani Robert Nesta Marley, Bob Marley kwa umaarufu. Mzungumzaji wa taratibu aliyeamini katika imani ya kirastafari. Aliingia katika mgogoro na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Jamaica Michael Manley.

Akiwa nyumbani kwake mwezi December 1976 akijiandaa kutumbuiza tamasha la muziki alipigwa risasi, hazikumuua na watuhumiwa hawakupatikana. Bob Marley alimtuhumu waziri mkuu wa wakati huo kwa tukio hili.

Bob Marley, umeondoka lakini muziki wako unaishi na unabeba yote kila mmoja anayotaka kusikia leo na kesho.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…