Mshana Jr nadhani alishawahi kuliongelea hili. Kama sikosei ni yale mambo ya kuuhama mwili na kwenda sehemu zingine kiroho na inasemekana ndiyo njia ambayo hutumiwa na wachawi na wengineo kuingia majumbani huko bila kufungua milango na madirisha. Ni hatari kidogo hasa kwa watu wanaoanza kwa sababu ukikosea kidogo tu basi unakufa. Tena inabidi ufanyie mahali patulivu kwa sababu ikitokea mtu akaushtua mwili uliouacha kabla hujapata muda wa kuurudia basi hutaweza kurudi tena na hivyo unafariki.
Google Astral projection kama unataka kujifunza zaidi na kuna video nyingi YouTube. Hata hapa JF mada hii ilishaongelewa sana. Dunia hii ina mambo mengi yasiyojulikana...