Makapuku Forum

ZABURI 4

8 Katika Amani nitajilaza na kupata usingizi mara,Maana wewe , BWANA peke yako,ndiye unijaliaye kukaa salama.

USIKU MWEMA MBARIKIWE
Usiku mwema kwako pia. Njozi njema


Ushauri wa bure: Ni vizuri kukojoa kabla ya kulala, unaweza kukojoleshwa ndotoni

Ushauri huu umetolewa na anko wangu, unajua kabisa mimi siwezi kukuandikia mambo haya
 
Zaburi 143

11 Ee BWANA, unihuishe kwa ajili ya jina lako, Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

12 Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.
 
Huu wimbo dedication kwa kikongwe wangu popote ulipo dunian, japo sikujui.
 
Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa Majeshi Asante kwa Upendo wako na kutuamsha tukiwa wazima na Afya njema,wapo watu wengi walitamani kuiona siku ya leo Baba hawajaweza ,tunatoa Sifa ,Shukurani,Heshima na Utukufu kwa Neema hii.

Tunakuja Mbele zako tukikukabidhi siku ya leo ya Jumatano 8 Novemba 2017 ikawe njema na ya kukupendeza.
Tunaomba toba kwa yote tuliyokosea.Kwa mawazo ,maneno na matendo Uturehemu twakusihi
Tuimarishe ili tukupende,tukuheshimu na kuishi maisha ya kukupendeza wewe tu.
Tunaikabidhi Nchi yetu iwe na Amani.
Tunazikabidhi Familia zetu zidumishe Upendo na Mshikamano.
Tunawakabidhi wagonjwa na wenye shida mbalimbali majumbani na mahospitalini Baba ukawaponye miili na roho pia.
Baba wasafiri wote majini,nchi kavu,angani ukawe nao waende na kurudi salama.Na familia zote Baba mwema zikawe salama na Amani itawale.
Watoto wetu popote walipo makazini,majumbani na mashuleni ukawasimamie wakawe vichwa si mikia wafanye mambo yote kwa ufanisi na mafanikio.
Baba Mungu tunazikataa kazi zote za shetani zisipate nafasi katika maisha yetu tunazivunja kazi zote za shetani katika jina la Yesu Kristo tunamwaga damu ya Yesu Kristo ikatakase kila pando na kuling'oa na kulitupa kuzimu Mfalme wa Amani.
Tunakabidhi kazi zote za mikono yetu zikapate kibali mbele yako nawale wasio na kazi na shughuli za kufanya Baba wape kazi ili wauone Utukufu wako, tuingiapo na kutoka utubariki.
Baba Asante kwa Matendo yako Makuu yasiyo na mwisho,tunauona ukuu wako siku zote za maisha yetu tunasema Asante Baba na tunaomba uzidi kutuimarisha imani zetu zipande kuwa viwango vya juu ili tuweze kushuhudia matendo yako siku hadi siku.Roho Mtakatifu tutie nguvu.
Nakushukuru maana utatenda yote sawa na mapenzi yako
Katika jina la Yesu Kristo naomba naamini na nashukuru Amen


SIKU NJEMA WAPENDWA MBARIKIWE
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…