Makapuku Forum

Karibu katika Amka Na BBC.


- Hakuna dalili za suluhu kwa mzozo wa kisiasa Kenya

- Mashirika ya misaada yanaonya kuwa switafahamu ya uchaguzi Kenya imesababisha ukame kusahaulika

- Vijana wakusanyika polisi Kampala kaskazini, kudai kuachiliwa huru kiongozi wa upinzani Dr. Kizza Besigye

- Polisi Tanzania yashutumiwa kwa kuwakamata wana harakati 12 kwa madai ya kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja
 
1 Petro 4:7-11
[7]Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.
[8]Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.
[9]Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika;
[10]kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.
[11]Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.



SIKU NJEMA WAPENDWA...MBARIKIWE
 
TUOMBE:
UHIMIDIWE JEHOVA MFALME.
Ahsante kwa ulinzi wako kwa usiku kucha.
Tubariki Bwana.
Leo tukawe mikononi mwako.
Poza wauguao, Fariji wenye huzuni, Leta Umoja Upendo na Amani kwa watu wako.
Malaika wako na wakafanye kituo kwa kila mtu , tuingiapo na tutokapo.
Simamia kila jambo Mfalme wa Amani,bariki kazi za mikono yetu,bariki familia zetu ,bariki watoto wetu,bariki mipango yetu.
Naomba ni katika Jina la Yesu Amina

SIKU NJEMA KWENU WOTE MBARIKIWE
 
Leo nimeanza siku vizuri,mara paaaaaap mama mchungaji huyu hapa anamwaga upako. Habari ya siku mingi
 
Amen


Ubarikiwe sana mama mchungaji
 
Amina mama
 
Amen mama mchungaji, nawe pia siku njema
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…