Makapera mna nini kwani raha hampendi?

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
2,537
2,530
Usiku umeingia, wakubwa kaeni chonjo.
Ninataka wamwagia, mvizidishe vionjo.
Watoto kujilalia, wakongwe wapewe chanjo.
Makapera mna nini, kwani raha hampendi?
Kucha mwajikumbatia, baridi linalindima.
Maradhi yawazidia, hali ndoa jambo jema.
Moyoni mwajililia, mwajitia uyatima.

*Makapera mna nini, kwani raha hampendi?*


Mifano twawapigia, dhahiri yaonekana.
Nyoyo zetu zatulia, wenzetu tukiwaona.
Masingo mwayasikia, hamjawahi yaona.

*Makapera mna nini, kwani raha hampendi?*

Waulize walooa,,raha wazojipatia
Njiani wapata karaha,,nyumbani waenda poa
Riziki zao kwa Mola,,dhima amejibebea

KAPERA MACHO FUMBUA,,WAULIZE WALOOA

Tazama raha yandoa,,kwa waliojiolea
Nyumbani akirejea,,home aja kumbatiwa
Dikodiko kapikiwa,,na Nguo kufuliwa

KAPERA FUMBUA MACHO,,WAULIZE WALOOA




Macho wameyakodoa, upofu wanaigiza.
Lawama wanazitoa, juhudi wamefifiza.
Dua tunawaombea, waondoke kwenye giza.

Makapera mna nini, kwani raha hampendi?

```Mahari si lazima pesa, hata kanga inafaa.
Macho muache pepesa, acheni kutuhadaa.
Bure bure mwajitesa, mwishowe mtadumaa. ```

Makapera mna nini, kwani raha hampendi?

Wakuu kipengele cha Uchambuzi wa Maudhui nawaachia mjidada vulie Dhamira zilizopo kwenye Shairi letu la Leo

Nawasilisha..............!!!!!
 
Back
Top Bottom