Makao makuu ya Wilaya ya Kilombero

lnx

JF-Expert Member
Oct 21, 2016
387
294
Naomba kuuliza au kuelekezwa kuna vigezo gani hufuatwa ili makao makuu ya wilaya yaweze kujengwa mahala fulani?

Nimeuliza hilo sababu kuna sintofahamu wapi makao makuu ya Wilaya ya Kilombero yawekwe japo kwenye kikao cha madiwani walikubalina yawe Mngeta ambapo kimsingi ndiyo katikati ya wilaya hiyo tofauti na yanakotaka kupelekwa pembeni kabisa, lisaa limoja unaingia Wilaya ya Mikumi sijui kama mko sahihi.

Yaani ili ufike ofisi za Halmashauri ya Kilombero sharti upite katikati ya Halmashauri ya Mji Ifakara wakati sehemu kubwa imeachwa kwenda hadi mlimba huko na ndiyo ilikuwa imepangwa yawe mlimba leo mnayapeleka huko siginari kulikoni?

Nia ya raisi ni kusogeza huduma kwa watu leo mnataka mtu wa mlimba watembee masaa 6 au 7 na mvua zikinyesha ndiyo watasafiri siku nzima kufuata huduma wilayani hii imekaaje.

Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wako hapa inatakiwa mjitathimini hicho mnachotaka kukufanya hakina unafuu wala msaada wowote kwa raia wenu walioko masagati au mlimba kama lengo la Rais lilivyo.
 
Hili swala naona Siasa zimetawala Sana, mbunge wetu Kiwanga yeye anataka makao makuu yaende kwao mlimba, huku wengine wanataka yaende mngeta na wengine wanataka yaenda huko Mang'ula...

Ukweli Ni na uhalisia MNGETA ni mahali sahihi Sana, rahisi kufikika na miundombinu inaruhusu kbsa!! Tuache Siasa, tuache madaraka( classes), tuache tofauti zetu, wananchi tunataka maendeleo tu, tuleteeni halmashauri Mngeta km kikao Cha Baraza la madiwani walivyoazimia
 
Hawahusiki kwani hawa?
Hao ni viongozi tu,kama wataleta uchama kwenye hoja ya msingi hii hawatakuwa na nia njema ya kuwasaidia hawa wakazi wa huku mngeta-mlimba balia wanataka kuwakomoa.
Inakuwaje sehemu kubwa ya wilaya ya inaachwa pembeni halafu unapeleka makoa makuu ya wilaya karibia na wilaya nyingne mfano mikumi na hapo bado ili ufike ofisi za halimashauri lazima upite halimashauri ya mji ifakara.
Hapa watawala mnataka kuyumba,ondoweni u-ccm na u-chadema wenu muwasogezee wananchi huduma.
 
Suluhisho sahihi ni kuwa wilaya ya Kilombero igawanywe ili zipatikane wilaya mpya tatu kwani ni kubwa sana:
1.Wilaya ya Kilombero-Makao Makuu yawe aidha Mang'ula au Kiberege.
2.Halmashauri ya Mji was Ifakara-Makao makuu yake yawe mjini Ifakara.
3.Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba-Makao yake Makuu yawe Mlimba.
MWISHO: Mkoa wa Morogoro nao ugawanywe haraka sana ili ipatikane mikoa miwili, yaani Mkoa wa Morogoro na kuunda Mkoa mpya wa Ulanga, ambao makao yake Makuu ya Mkoa mpya yawe mjini Ifakara.
 
Suluhisho sahihi ni kuwa wilaya ya Kilombero igawanywe ili zipatikane wilaya mpya tatu kwani ni kubwa sana:
1.Wilaya ya Kilombero-Makao Makuu yawe aidha Mang'ula au Kiberege.
2.Halmashauri ya Mji was Ifakara-Makao makuu yake yawe mjini Ifakara.
3.Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba-Makao yake Makuu yawe Mlimba.
MWISHO: Mkoa wa Morogoro nao ugawanywe haraka sana ili ipatikane mikoa miwili, yaani Mkoa wa Morogoro na kuunda Mkoa mpya wa Ulanga, ambao makao yake Makuu ya Mkoa mpya yawe mjini Ifakara.
Kikwazo itakuwa idadi ya watu

Mkoa wa Morogoro hauna population kubwa
 
Kikwazo itakuwa idadi ya watu

Mkoa wa Morogoro hauna population kubwa
Sina uhakika na hii hoja kuwa mkoa wa morogoro hauna watu,lakini kikubwa hii wilaya ya kilombero bora ikagawanywa maana mlimba ni parefu sana kutoka ifakara mji,mwendo wa masaa zaidi ya matano
 
Back
Top Bottom