Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega.
[FONT=ArialMT, sans-serif]Serikali mkoani Kilimanjaro, imesema kamwe haitawavumilia makandarasi wanaokwenda kinyume na mkataba wa ujenzi wa barabara kwa kuchelewa kukamilisha kazi au kujenga chini ya kiwango.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Vile vile, imesisitiza azma yake ya kuchukua hatua za[/FONT] [FONT=ArialMT, sans-serif]kisheria mara moja kwa makandarasi wababaishaji[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]wenye lengo la kujipatia fedha za walipa kodi bila kujenga barabara kwa kiwango kinachotakiwa na kwa mujibu wa mkataba kazi walizopewa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mkuu wa Mkoa huo, Monica Mbega, aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa ujenzi barabara nne za kiwango cha lami za Kwasadala-Masama, Kibosho-Sinde-Kwa Rafaeli-Internation School, Rau Madukani-Uru Njari na KawawaNduoni-Marangu Mtoni katika wilaya za Hai na Moshi Vijijini ikiwa ni utekelezaji wa ahadi za Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni za[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]uchaguzi mwaka 2005.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alimuagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Kilimanjaro kushirikiana na mhandisi mshauri kufuatilia mara kwa mara ujenzi wa barabara hizo ili uwe wa kiwango na kuepusha gharama zisizo za msingi[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]kwani kuchelewesha au kubadili badili hakuvumiliki.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Awali, katika taarifa yake, Meneja wa Tanroads mkoani Kilimanjaro, Tumaini Sarakikya, alisema barabara hizo zina urefu wa kilomita 80.1 na kwamba hadi sasa zimetumia zaidi ya Sh. milioni 497.8 kwa ajili ya usanifu kwa mwaka wafedha 2008/09.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sarakikya alisema barabara ya Kibosho Shinde-Kwa[/FONT] [FONT=ArialMT, sans-serif]Raphael-Internation School (27.5), imejengwa kwa kiwango cha lami kwa kilomita nne kwa zaidi ya Sh. billion 1.9. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hadi sasa zaidi ya Sh. billion 2.4 zimetumika.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alizitaja barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami na idadi ya kilomita kwenye mabano kuwa ni Kwasadala-Masama (12.5).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Nyingine ni Rau Madukani-Uru Njari (9.5) na Kawawa Nduoni-Marangu Mtoni (30.6). [/FONT]
CHANZO: NIPASHE