Makamu wa Raisi Dkt MPANGO Aagiza Homilia hii ya Askofu mkuu jimbo katoliki la Mbeya Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga Irudiwe kwenye Vyombo vya Media ya Serikali
View: https://m.youtube.com/watch?v=h483w5Qe2fI
Habari kamili :
Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga ambaye katika mahubiri yake amesema Baba wa Taifa alikuwa ni mtu aliyefuata maadili mema ikiwemo mwenendo haki, huruma, unyenyekevu na uaminifu.
utakatifu hujulikana kwa mtu aliyeishi bila kufanya uovu...
Uadilifu wa ndani, moyo ulio kataa kutenda dhambi, mtu mwenye huruma, mpenda haki
Watu wote bila kujali dini zao rangi wanatakiwa na Mungu kuishi kwa kutofanya maovu
Uchunguzi wa maisha ya mtu huyo muadilifu hufanywa na watu walioishi naye, ...
Amesema Mwalimu Nyerere aliacha urithi wa kisiasa tangu wakati wa kuhangaikia uhuru, aliacha urithi wa Muungano wa Taifa pamoja na mageuzi ya kidemokrasia. Pia amesema kupitia Azimio la Arusha mwaka 1967 Mwalimu Nyerere aliacha urithi wa kijamii na kiuchumi ili kujenga jamii yenye usawa.
Askofu Mkuu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga ameongeza kwamba, Mwalimu Nyerere alisisitiza elimu kwa lengo la kuondoa ujinga na kuweza kujitegemea, aliacha urithi wa utamaduni hususani kwa kusisitiza matumizi ya lugha ya Kiswahili, maadili na utu na aliweka maslahi ya Taifa mbele.
Pia amesema Baba wa Taifa alitoa mchango wa ukombozi wa kikanda na kimataifa kupitia usaidizi wake katika kuhakikisha mataifa mengine yanakuwa huru. Alitoa mchango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, kushiriki kujenga diplomasia ya kusini mwa Dunia na kupigania usawa wa kiuchumi kati ya mataifa matajiri na mataifa yanayoendelea.
Amesema kupitia jitihada hizo na nyingine nyingi, ni hamasa kwa Watanzania kuendelea kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili aweze kusamehewa makosa yake na kuwa Mwenyeheri.
Ibada hiyo pia imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali.