Makamu wa Rais wa Sudan Kusini amshukuru JK

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,292
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akizungumza na Makamu wa Rais wa Sudani Kusini Riek Machar mjini Addis Ababa, Ethiopia mwishoni Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Chanjo.

Katika mazungumzo hayo, Makamu huyo wa Rais alimshukuru Rais Mstaafu Kikwete kwa mchango ambao CCM imeutoa katika kusuluhisha mgogoro ndani ya chama tawala cha SPLM hadi kufikiwa kwa makubaliano ya Arusha. Ametumia pia fursa hiyo kuomba CCM kuendelea kukisaidia chama cha SPLM kutokana na uzoefu na ukomavu wake wa uongozi.

Amemhakikishia Rais Mstaafu Kikwete juu ya azma yake ya kurejea Juba mapema iwezekanavyo.
Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete amempongeza kwa utayari wake wa kurejea Juba na amemuhakikishia kuwa CCM haitatupa mkono SPLM na itaendelea kushirikiana na kutoa mchango wake pale utakapohitajika

Kikwete akutana na Riek Machar jijini Addis Ababa - wavuti
 
Jpm azingatie kujenga uchumi na kuzuia wizi wa ndani na nje pia aendelee kupambana na wauza unga! Sifa nyingine hazitusaidii,kuna rais alikua anahangaika kumtafutia damond eti connection za mziki marekani!!! Mambo ya ajabu kabisa,nchi inahujumiwa wizi kilasekta rais yukobusy na vituko vya ajabu
 
N
Hatar sanaa
 
Back
Top Bottom