Makamu wa Rais ni Mdomo umeteleza au?

Makamu wa Rais ni Mdomo umeteleza au?

yaani ni wewe usiyeelewa tatizo liliopo hivi Zanzibar na ndio maana unaweka mijadala ya ajabu ajabu hapa au kuipindisha iliyopo.
Kama unalielewa Tatizo la Znz ni vyema ukajibu kwa hoja sio kurukaruka,

Hebu fafanua Mwenyekiti wa ZEC ana uhalali wakufuta uchaguzi?

Je Waliopiga kura Znz si ndio hao hao waliopiga kura za Ubunge na Urais wa JMT?
 
yaani wewe Anko utanikatisha usingizi wangu nikianza kutoa darsa. OK faini b......mbili. Kuna time ya jecha Zechariah inashughulikia uchaguzi was Raiss Zanzibar, wawakilishi na madiwani-madanduku matatu hayo . Kuna time. ya jaji luniva NEC nashughulilia uchaguzi was Rais t na wabunge- masanduku Mengine mawili hayo. hivyo wazanzibari 25 oktoba wamejaza lura tano kwa masamduku hayo matano na wasimamizi ni NEC na zec vyombo ambavyo kila kimoja kiko vyake na kinajitegemea kwa mujibu wa sheria
Znz kulikuwa na watendaji wa NEC?
 
Kama huelewi mambo nyamaza Makamu wa Rais wa Jmt hahusiki na Siyo tunda au zalio la uchaguzi wa Zanzibar unaosimiwa na Zec ya Jecha.

Sasa nawe unachanganya mambo ataachaje kuwa zao la uchaguzi wa Zanzibar na wakati jaji Lubuva amejumlisha kura za huko ?????????!! Na lubuva kasema hazina kasoro yoyote ???!
 
Sasa nawe unachanganya mambo ataachaje kuwa zao la uchaguzi wa Zanzibar na wakati jaji Lubuva amejumlisha kura za huko ?????????!! Na lubuva kasema hazina kasoro yoyote ???!

wazanzibari wamepiga kura masanduku matano. mawili yanasimamiwa na NEC ya jaji lubuva, ndiyo hayo aliyoisabu kwa kuwa hakuyaona na kasoro. masanduku mengine matatu yalisimamiwa na zec ya Jecha na ndo hayo yaliyokuwa na vimbwanga had I Jecha akafikia hatua ya kufuta matokeo.
 
Hivi nyinyi mkoje great thinkers wa JF. mnasikiliza vitu na ku-digest kama ni wanafunzi wa Sekondari? Hakuna issue hapo na hakuna kasoro. yupo sahihi. acheni Fujoo zenu- tafadhal

Kwani yeye ni makamu wa rais wa JMT au wa Tanzania bara?
 
wazanzibari wamepiga kura masanduku matano. mawili yanasimamiwa na NEC ya jaji lubuva, ndiyo hayo aliyoisabu kwa kuwa hakuyaona na kasoro. masanduku mengine matatu yalisimamiwa na zec ya Jecha na ndo hayo yaliyokuwa na vimbwanga had I Jecha akafikia hatua ya kufuta matokeo.

Hayo masanduku mawili kura zake zimehesabiwa na kusimamiwa na nani kama si ZEC YA JECHA kama wakala wa NEC . Kwa maana ya kuwa Lubuva anakusanya matokeo ya JMT toka kwa Jecha na watu wake. Na wapiga kura ni walewale @ moja kura tano.

Tabu yenu mnaoshabikia serikali na CCM nikuunga mkono hata mambo ya hila ili mfurahishe nafsi zenu bila kujali ya kesho.

Zamani hila hizohizo walitumia ki Sultan ASP(CCM) ilikuwa ikishinda uchaguzi lakini haitangazwi mshindi kisa hawakuwa na DOLA na walikuwa MALOFA the same thing leo ZEC na CCM yake wanaifanyia CUF. huo nao ni USULTANI
 
Hoja ya msingi inabaki palepale kwani lowasa ?liposema ccm oyee kwenye kampeni za ukawa alimaanisha hivyo?
 
yaani wewe Anko utanikatisha usingizi wangu nikianza kutoa darsa. OK faini b......mbili. Kuna tume jecha inashughulikia uchaguzi wa Rais Zanzibar, wawakilishi na madiwani-madanduku matano hayo. Kuna tume ya jaji lubuva NEC nashughulikia uchaguzi wa Rais na wabunge- masanduku Mengine mawili hayo. hivyo wazanzibari 25 oktoba wamejaza kura tano kwa masanduku hayo matano na wasimamizi ni NEC na zec vyombo ambavyo kila kimoja kiko vyake na kinajitegemea kwa mujibu wa sheria
Ok, sasa nipe darasa WZN wanachaguaje Rais wa JMT
Kulikuwa na vituo tofauti kwamba mtu akimaliza kituo cha ZNZ anatoka nje na kwenda kituo cha JMT?

 
Wakuu,

Muda Mfupi uliopita nimemsikia Makamu wa Rais wa JMT,Wakati akiongea katika kongamano la Wanawake wanasiasa,Akisema kuwa Uchaguzi wa Tanzania bara ulimalizika salama ila Wa Zanzibar ulikuwa na Matatizo na Juhudi zinaendelea kufikia muafaka wa uchaguzi huo.

Mtazamo wangu hapa Najiuliza Makamu wa Rais ameteleza au hatambui kuwa hakuna uchaguzi wa Tanzania bara bali wa Rais wa JMT na ule wa Zanzibar?

CC-@Nguruvi3 Pasco Mchambuzi, Mkandara.

======================



Chanzo: ITV
Mbona hii ninya kawaida sana simkwa watu wa Tanzania bara na hasa hasa wa Zanzibar kwa vyama vyote kufikiria Serikalimya Muungamomni Serikalinya Tanzania bara. Kiuhalisia hii ndivyo ilivyo serikali ya muunganomkwa sehemu kubwa inashughulika na mambo ya bara tu.
 
Back
Top Bottom