Makamu wa Rais ni Mdomo umeteleza au?

Makamu wa Rais ni Mdomo umeteleza au?

sidhani kama ameteleza.
Kwa uelewa wa chama chake, Uchaguzi ZNZ urudiwe. Maana yake kura za Rais wa JMT zina walakini

Hoja wasioelewa wengi ni kuwa WZNZ wanapiga kura 5.
Sasa kama watu walikuwa wengi kuliko walivyoandikishwa, basi hata kura za Rais wa JMT zina matatizo.

Nadhani makamu yupo sahihi, kwamba Rais ni wa bara kwa msingi kuwa uchaguzi kule ulivurugwa

Hapa sasa sijui ndiko kuteleza au! maana anaweka mambo kuwa magumu kwa Rais wa JMT
Mkuu, Nguruvi3 Kwa nafasi yake kama Makamu wa Rais,Anaturudisha kule kule kuhusiana na Msukumo uliomfanya Mwenyekiti wa ZEC Kufuta uchaguzi wa Znz ilihali kisheria akikosa uhalali huo.

Inaonekana kufutwa kwa uchaguzi wa Znz kulifanywa kwa kukurupuka kutokana na hamaki ambyo sasa inatia doa uhalali wa JPM kikatiba.
 
Last edited by a moderator:
Hivi nyinyi mkoje great thinkers wa JF. mnasikiliza vitu na ku-digest kama ni wanafunzi wa Sekondari? Hakuna issue hapo na hakuna kasoro. yupo sahihi. acheni Fujoo zenu- tafadhal

Pakacha,

Ni vyema ukafafanua huo usahihi ambao unaujua wewe kuhusiana na Uchaguzi wa Tanzania bara.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, Nguruvi3 Kwa nafasi yake kama Makamu wa Rais,Anaturudisha kule kule kuhusiana na Msukumo uliomfanya Mwenyekiti wa ZEC Kufuta uchaguzi wa Znz ilihali kisheria akikosa uhalali huo.

Inaonekana kufutwa kwa uchaguzi wa Znz kulifanywa kwa kukurupuka kutokana na hamaki ambyo sasa inatia doa uhalali wa JPM kikatiba.
Yaani Jecha kawaweka mahala pagumu sana.

CCM wakisema Rais JMT kachaguliwa kihalali basi matokeo yatangazwe ZNZ
CCM wakisema uchguzi urudiwe, wabunge wa ZNZ wanafutika , baraza la mawaziri linakuwa la Tanganika

Haya ni matokeo ya kuongoza nchi kwa 'ndiyoooooo'' na kudai Toyota mkonga. Ni matokeo ya CCM ile ile kuwa na kiburi cha kutawala tu bila maarifa. La ZNZ litatueleza zaidi maana hawana pa kutokea
 
Wakuu,

Muda Mfupi uliopita nimemsikia Makamu wa Rais wa JMT,Wakati akiongea katika kongamano la Wanawake wanasiasa,Akisema kuwa Uchaguzi wa Tanzania bara ulimalizika salama ila Wa Zanzibar ulikuwa na Matatizo na Juhudi zinaendelea kufikia muafaka wa uchaguzi huo.

Mtazamo wangu hapa Najiuliza Makamu wa Rais ameteleza au hatambui kuwa hakuna uchaguzi wa Tanzania bara bali wa Rais wa JMT na ule wa Zanzibar?

CC-@Nguruvi3 Pasco Mchambuzi, Mkandara.

Siyo hivyo tu, kasema uchaguzi wa Zanzibar utarudiwa.. Inaonekana ccm wameshajipanga kwa hilo tayari iki kulazimisha marudio huku wakizuga na mazungumzo feki!!
 
Last edited by a moderator:
Yaani Jecha kawaweka mahala pagumu sana.

CCM wakisema Rais JMT kachaguliwa kihalali basi matokeo yatangazwe ZNZ
CCM wakisema uchguzi urudiwe, wabunge wa ZNZ wanafutika , baraza la mawaziri linakuwa la Tanganika

Haya ni matokeo ya kuongoza nchi kwa 'ndiyoooooo'' na kudai Toyota mkonga. Ni matokeo ya CCM ile ile kuwa na kiburi cha kutawala tu bila maarifa. La ZNZ litatueleza zaidi maana hawana pa kutokea

Kama huelewi mambo nyamaza Makamu wa Rais wa Jmt hahusiki na Siyo tunda au zalio la uchaguzi wa Zanzibar unaosimiwa na Zec ya Jecha.
 
Siongeleo makamu wa Rais wa JMT, Naongelea Rais wa JMT

Kauli ya Makamu wa Rais ndiyo inazua maswali. Yeye hapigiwi kura m umeelewa

Tulia ufuatilie mjadala kwanza uelewe hoja imetoka wapi na inakwenda wapi.
 
Nguruvi3,

Ndiooo! Ukijumlisha na Utamaduni wa watawala kucheza na akili za Watanzania ambao kimsingi wanashindwa kusimamia mahitaji yao inakuwa Janga kwa Taifa.

Kwa mfano ukiangalia ustadi unaotumiwa kuteka Mijadala katika Media unatambua Jinsi ambvyo maswala muhimu ikiwemo la Znz livyojaribu kuwekwa Pembeni kimkakati.
 
Last edited by a moderator:
Kama huelewi mambo nyamaza Makamu wa Rais wa Jmt hahusiki na Siyo tunda au zalio la uchaguzi wa Zanzibar unaosimiwa na Zec ya Jecha.
Ni vyema kama hujaelewa Mjadala ukaomba kueleweshwe Ndugu!
 
Nguruvi3,

Ndiooo! Ukijumlisha na Utamaduni wa watawala kucheza na akili za Watanzania ambao kimsingi wanashindwa kusimamia mahitaji yao inakuwa Janga kwa Taifa.

Kwa mfano ukiangalia ustadi unaotumiwa kuteka Mijadala katika Media unatambua Jinsi ambvyo maswala muhimu ikiwemo la Znz livyojaribu kuwekwa Pembeni kimkakati.
Hizi mbwembwe zote zinazofanyika za kufukuza watu, kuzuia matumizi n.k. ni njama za kuondoa watu kutoka kwenye hoja

Hawataki kabisa suala la ZNZ kwasababu lina ncha mbili

Kwanza, linawaumbua kama vinara wa demokrasia. Leo tutakwenda nchi gani kusuluhisha ikiwa wenyewe

Pili, lazima litagusa NEC na jinsi Rais wa JMT alivyochaguliwa
 
Siongeleo makamu wa Rais wa JMT, Naongelea Rais wa JMT

Kauli ya Makamu wa Rais ndiyo inazua maswali. Yeye hapigiwi kura m umeelewa

Tulia ufuatilie mjadala kwanza uelewe hoja imetoka wapi na inakwenda wapi.

Sawa Rais wa Jmt huwezi kumhusianisha na uchaguzi wa Zanzibar unaoratibiwa. na kusimamiwa na zec ya Jecha wake yeye ni ule uliosimamiwa na kuratibiwa na NEC ya Jaji Lubuva
 
Tueleze, wznz wanapigaje kura ! Tuanzie hapo
 
yaani ni wewe usiyeelewa tatizo liliopo hivi Zanzibar na ndio maana unaweka mijadala ya ajabu ajabu hapa au kuipindisha iliyopo.
 
yaani wewe Anko utanikatisha usingizi wangu nikianza kutoa darsa. OK faini b......mbili. Kuna tume jecha inashughulikia uchaguzi wa Rais Zanzibar, wawakilishi na madiwani-madanduku matano hayo. Kuna tume ya jaji lubuva NEC nashughulikia uchaguzi wa Rais na wabunge- masanduku Mengine mawili hayo. hivyo wazanzibari 25 oktoba wamejaza kura tano kwa masanduku hayo matano na wasimamizi ni NEC na zec vyombo ambavyo kila kimoja kiko vyake na kinajitegemea kwa mujibu wa sheria
 
Back
Top Bottom