Alexandry Nemesi
JF-Expert Member
- Jun 7, 2014
- 1,508
- 590
Wakuu,
Muda Mfupi uliopita nimemsikia Makamu wa Rais wa JMT,Wakati akiongea katika kongamano la Wanawake wanasiasa,Akisema kuwa Uchaguzi wa Tanzania bara ulimalizika salama ila Wa Zanzibar ulikuwa na Matatizo na Juhudi zinaendelea kufikia muafaka wa uchaguzi huo.
Mtazamo wangu hapa Najiuliza Makamu wa Rais ameteleza au hatambui kuwa hakuna uchaguzi wa Tanzania bara bali wa Rais wa JMT na ule wa Zanzibar?
CC-@Nguruvi3 Pasco Mchambuzi, Mkandara.
======================
Chanzo: ITV

Makamu wa rais Mh Samia Hassan Suluhu amewataka wanawake nchini kuwa kitu kimoja.
Makamu wa rais Mh Samia Hassan Suluhu amewataka wanawake nchini kuwa kitu kimoja wanapopigania ajenda zao badala ya kukatishana tamaa na kubezana huku akiahidi kushughulikia kwa nguvu zote kero zinazowagusa wanawake.
Mh Suluhu ametoa wito huo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na ulingo wa wanawake wanasiasa ambapo amesema kikwazo kikubwa cha wanawake ni wanawake wenyewe kwa kuwa wakwanza kuvunjana moyo na kunyimana haki.
Kuhusu mgogoro wa Zanzibar Mh Suluhu amesema viongozi wanajitahidi kupata suluhu kwani tatizo la upande mmoja ni la pande zote mbili na kuwataka wanawake kuungana kuhakikisha Zanzibar inakaa sawa.
Akimkaribisha makamu wa rais mwenyekiti wa ulingo huo Bi Anna Abdalah amesema licha ya changamoto nyingi zinazowakabili wanawake pamoja na baadhi yao kupata majeraha ya uchaguzi lakini wamebeba ajenda ya amani na ndiyo maana wameweza kukutana bila kujali itikadi za vyama vyao.
Baadhi ya wanawake waliohudhuria wakiwemo wanaharakati wamesema matarajio yao ni kwamba ajenda ya wanawake itafanyiwa kazi hasa suala la demokrasia ndani ya vyama vya siasa huku wakimweleza matatizo mbalimbali wanawake wanayokutana nayo yakiwemo ya ukatili wa kijinsia.
Chanzo: ITV
Last edited by a moderator: