Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi asisitiza umuhimu wa kulinda mazingira na muungano

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
𝗧𝗔𝗔π—₯π—œπ—™π—” π—žπ—ͺ𝗔 𝗩𝗬𝗒𝗠𝗕𝗒 𝗩𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗕𝗔π—₯π—œ

π— π—”π—žπ—”π— π—¨ π—ͺ𝗔 π—₯π—”π—œπ—¦ π—”π—¦π—œπ—¦π—œπ—§π—œπ—­π—” π—¨π— π—¨π—›π—œπ— π—¨ π—ͺ𝗔 π—žπ—¨π—Ÿπ—œπ—‘π——π—” π— π—”π—­π—œπ—‘π—šπ—œπ—₯𝗔 𝗑𝗔 π— π—¨π—¨π—‘π—šπ—”π—‘π—’

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia dhamana kubwa waliyopewa ya kusimamia suala la Mazingira na Muungano hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira katika kikao kazi kilichofanyika mkoani Dodoma. Amewataka kutambua na kuchukulia kwa uzito suala la uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwani linabeba mustakabali wa vizazi vya sasa na baadaye.

Aidha amewataka kuwa na utaratibu wa upimaji wa malengo yaliyowekwa katika Wizara hiyo ikiwemo upandaji wa miti ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango na malengo ya uhifadhi mazingira yanakuwa na matokeo mazuri na yenye manufaa.

Makamu wa Rais, amesema ni lazima Wizara hiyo kutambua umuhimu wa suala la Muungano kwa kuhakikisha elimu inatolewa vya kutosha kwa wananchi hususani vijana kwa kuhusianisha maendeleo na mafanikio ya Taifa yanategemea uimara wa Muungano.

Ameongeza kwamba, kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliozaliwa baada ya Muungano mwaka 1964, ni vema kutoa elimu ya kuwafahamisha umuhimu na uzuri wa Muungano ili kuweza kuendeleza yale ya Serikali zilizopita na kuwa na Taifa zuri zaidi kwenda mbele.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa Wizara hiyo kujipanga kuhakikisha inatekeleza hapa nchini, maazimio na mipango ya kulinda mazingira yanayofikiwa katika mikutano ya kimataifa ambayo Tanzania inashiriki.

Vilevile, Makamu wa Rais amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuzingatia ahadi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwa kubainisha yale yanayohusu Wizara hiyo na yatekelezwe kwa ufanisi.

Makamu wa Rais amewasihi watumishi hao, kuisoma na kuelewa vema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kubaini maeneo ambayo Wizara inahusika zaidi na kuhakikisha yanatekelezwa. Pia amewaagiza kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2025 - 2030 na kutekelezaa yale ambayo Wizara inahusika moja kwa moja.

Makamu wa Rais amewahimiza kuzingatia mafunzo kazini ili kuweza kuenda sambamba na mabadiliko yanayojitokeza pamoja na kufanya kazi kwa bidii na nidhamu na kuwa mfano mzuri katika Serikali.

Awali Makamu wa Rais, alitembelea na kukagua jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira linalojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma, na kupongeza hatua kubwa iliyofikiwa katika ujenzi huo na kuwasihi wakandarasi kuhakikisha wanatimiza ahadi ya kukamilisha jengo hilo ifikapo mwezi Machi 2026.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
05 Desemba 2025
Dodoma.
 
Attachments

  • IMG-20251206-WA0010.jpg
    IMG-20251206-WA0010.jpg
    107.9 KB · Views: 13
  • IMG-20251206-WA0005.jpg
    IMG-20251206-WA0005.jpg
    91.3 KB · Views: 8
  • IMG-20251206-WA0009.jpg
    IMG-20251206-WA0009.jpg
    80.3 KB · Views: 13
  • IMG-20251206-WA0008.jpg
    IMG-20251206-WA0008.jpg
    93.2 KB · Views: 10
  • IMG-20251206-WA0007.jpg
    IMG-20251206-WA0007.jpg
    109.1 KB · Views: 14
  • IMG-20251206-WA0004.jpg
    IMG-20251206-WA0004.jpg
    84.8 KB · Views: 9
  • IMG-20251206-WA0006.jpg
    IMG-20251206-WA0006.jpg
    84.3 KB · Views: 10
  • IMG-20251206-WA0002.jpg
    IMG-20251206-WA0002.jpg
    91.6 KB · Views: 7
  • IMG-20251206-WA0003.jpg
    IMG-20251206-WA0003.jpg
    102.5 KB · Views: 9
  • VID-20251206-WA0011.mp4
    21.4 MB
Muungano upi?
yaan watu mil 60+ watawaliwe na nchi nyingine ya watu mil 2?

Tanganyika viongozi ni viazi kweli!
 
Okay πŸ‘,
Kila kitu cha serikali ni mipango,
Pimeni Ardhi,
Nishati ya umeme nafuu ndio njia pekee yakunusuru mazingura.

Uzazi wa mpango Uzingatiwe kwa lazima.

Dira ya 2050 haifai , zaidi ni Kwa ajili ya kunufaisha Wana mtandao, millennium ili rizi 1 awe CEO.
 
Upuuzi mtupu eti Mh Balozi Dr 🀑

Ukishaona mtu anakuwa address namna hiyo most likely ni ujinga ujinga tu.
 
Kama ni maafande wapo lindo basi wamepeana mgongo, kila mtu ana target yake, naona jamaa amegarget kivyake
 
Nchi hii hatujafanya uchaguzi hatuna rais wala makamu.

Upuuzi wa ccm pelekeni kwenye ma group ya ccm.
 
𝗧𝗔𝗔π—₯π—œπ—™π—” π—žπ—ͺ𝗔 𝗩𝗬𝗒𝗠𝗕𝗒 𝗩𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗕𝗔π—₯π—œ

π— π—”π—žπ—”π— π—¨ π—ͺ𝗔 π—₯π—”π—œπ—¦ π—”π—¦π—œπ—¦π—œπ—§π—œπ—­π—” π—¨π— π—¨π—›π—œπ— π—¨ π—ͺ𝗔 π—žπ—¨π—Ÿπ—œπ—‘π——π—” π— π—”π—­π—œπ—‘π—šπ—œπ—₯𝗔 𝗑𝗔 π— π—¨π—¨π—‘π—šπ—”π—‘π—’

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia dhamana kubwa waliyopewa ya kusimamia suala la Mazingira na Muungano hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira katika kikao kazi kilichofanyika mkoani Dodoma. Amewataka kutambua na kuchukulia kwa uzito suala la uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwani linabeba mustakabali wa vizazi vya sasa na baadaye.

Aidha amewataka kuwa na utaratibu wa upimaji wa malengo yaliyowekwa katika Wizara hiyo ikiwemo upandaji wa miti ili kuhakikisha utekelezaji wa mipango na malengo ya uhifadhi mazingira yanakuwa na matokeo mazuri na yenye manufaa.

Makamu wa Rais, amesema ni lazima Wizara hiyo kutambua umuhimu wa suala la Muungano kwa kuhakikisha elimu inatolewa vya kutosha kwa wananchi hususani vijana kwa kuhusianisha maendeleo na mafanikio ya Taifa yanategemea uimara wa Muungano.

Ameongeza kwamba, kutokana na idadi kubwa ya wananchi waliozaliwa baada ya Muungano mwaka 1964, ni vema kutoa elimu ya kuwafahamisha umuhimu na uzuri wa Muungano ili kuweza kuendeleza yale ya Serikali zilizopita na kuwa na Taifa zuri zaidi kwenda mbele.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa Wizara hiyo kujipanga kuhakikisha inatekeleza hapa nchini, maazimio na mipango ya kulinda mazingira yanayofikiwa katika mikutano ya kimataifa ambayo Tanzania inashiriki.

Vilevile, Makamu wa Rais amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuzingatia ahadi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwa kubainisha yale yanayohusu Wizara hiyo na yatekelezwe kwa ufanisi.

Makamu wa Rais amewasihi watumishi hao, kuisoma na kuelewa vema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kubaini maeneo ambayo Wizara inahusika zaidi na kuhakikisha yanatekelezwa. Pia amewaagiza kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2025 - 2030 na kutekelezaa yale ambayo Wizara inahusika moja kwa moja.

Makamu wa Rais amewahimiza kuzingatia mafunzo kazini ili kuweza kuenda sambamba na mabadiliko yanayojitokeza pamoja na kufanya kazi kwa bidii na nidhamu na kuwa mfano mzuri katika Serikali.

Awali Makamu wa Rais, alitembelea na kukagua jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira linalojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma, na kupongeza hatua kubwa iliyofikiwa katika ujenzi huo na kuwasihi wakandarasi kuhakikisha wanatimiza ahadi ya kukamilisha jengo hilo ifikapo mwezi Machi 2026.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
05 Desemba 2025
Dodoma.
Kama hajazungumzia Maandamano ya D9 means yuko pamoja nayo,Kanisa liko nyuma yake
 
nchimbi acha upuuzi, huu muungano wa kijinga hivi??
1. mtanganyika hawezi kupata ajira zanzibar ila mzanzibar anaajirika tanganyika(shaka hamdu ni mkuu wa wilaya tanganyika)
2. mtanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar ila mzanzibar anajichotea tuu mahekari huku tanganyika
3. ukiwa unaenda zanzibar lazima uwe na kibali au kitambulisho, ila ukiwa mzanzibar huna haja ya hivyo?
4. mtanganyika hawezi kugombea nafasi yoyote zanzibar ila mzanzibar akiwa tanganyika anagombea cheo chochote bila shida .
5. n.k.......
huu ni usengeeee broooo hatuwezi kuendelea kuwq mafala kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom