ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo Mhe. Makamu wa Rais ataongoza wananchi wa Arusha na Mikoa ya jirani kesho katika kuaga miili ya wanafunzi, waalimu na dereva waliofariki katika ajali ya bus la Shule jana.
Pichani ni muonekano wa majengo ya Shule ya Lucky Vicent katika matokeo ya darasa la 7 mwaka 2016 Shule hii ilishika nafasi ya kwanza kati ya Shule 331 Kimkoa na nafasi ya 20 kati ya Shule 8109 Kitaifa. Jambo lilofanya wazazi wengi kupeleka watoto wao katika Shule hii.