Mama Mdogo
JF-Expert Member
- Nov 21, 2007
- 2,967
- 2,147
Kwa kweli Mama huyu kanifurahisha kwa kuagiza vyombo vya dola viwakamate wauaji ndani ya saa 24. Hata hivyo najiuliza, kwani wauaji kukamatwa ni mpaka isubiri amri ya Mheshimiwa Makamu wa Rais??? Swali la nyongeza, hivi wale wauaji wa Ndugu Mawazo walishakamatwa??
=======================
Mheshimiwa Makamu wa Rais Mama Suluhu Hassan leo ametembelea Wilaya ya Sengerema kata ya Sima ambapo usiku wa kuamkia jana kulifanyika mauaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja ya Mama na watoto wake kuuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Mhe. Makamu wa Rais Mama Suluhu Hassan ametoa masaa 24 kwa uongozi wa mkoa wa Mwanza pamoja na jeshi la polisi na vyombo vingine kuwatia nguvuni wale wote waliohusika na mauaji hayo.
Pichani ni makaburi yakiandaliwa kwa ajili ya kuzikwa kwa miili saba ya familia moja mapema leo Wilayani Sengerema .
Chanzo: Michuzi