Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amelitaka jeshi la polisi kushirikiana na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ili kupambana dhidi ya vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Dkt.Mpango ametoa kauli hiyo leo Agosti 11, 2025 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akifungua mkutano wa maafisa waandamizi wa jeshi la polisi nchini uliofanyika katika ukumbi wa shule ya polisi Moshi. Amesema wananchi wanatakiwa kuchagua viongozi kwa kuzingatia ilani za vyama vya siasa pamoja na uwezo halisi wa wagombea, kwani viongozi wanaopatikana kwa vitendo vya rushwa huathiri maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.