Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,439
- 6,692
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amewahakikishia Watanzania kwamba Chama hakina chuki wala kısası na mtu bali kinaamini kutekeleza sera ya maridhiano.
Wasira ametoa kauli hiyo jana akiwa katika mkutano wa hadhara alipokuwa akizungumza na wana CCM wilayani Urambo mkoani Tabora ambako anaendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, kuzungumza na viongozi wa CCM na kusikiliza kero za wananchi.
Alisema CCM inaamini katika maridhiano ambayo pia ni sera ya serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ndio maana hata Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu alipokuwa amekimbia nchi, maridhiano ndiyo yalimrudisha nchini.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Yule bwana mwenye kuuliza na wengine mliokuwa mnamsikiliza niwasaidie tu kuwaelimisha kwamba mkiwa na sera ya maridhiano haiwi mbadala wa sheria na wala huwezi kusema kwa sababu wewe ni mwenyekiti basi upo juu ya sheria.
Wote tuko chini ya sheria hata mimi nikiamka sasa hivi nikakupiga kofi, Jeshi la Polisi watanikamata hawawezi kusema wewe ni Makamu Mwenyekiti wa CCM maana umakamu haunipi uhuru wa kupiga watu makofi halafu nikaondoka salama.