Makampuni ya ujenzi wa makazi

Makampuni ya ujenzi wa makazi

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
2bd03fa89410c1fc750c64f056d1ea28.jpg

Katika nchi zilizoendelea miji hujengwa na makampuni ya ujenzi.

Moja ya shughuli zao ni kununua ardhi wakajenga kitongoji/mji wa kisasa. Chukulia eneo lote la Tabata lingekuwa limejengwa na kampuni ya ujenzi. Nyumba za kisasa na za mpangilio.

Na baadae kampuni hiyo huuza nyumba za eneo hilo au kuzikabidhi kwa mwenye mradi wake (mwekezaji)

Hivyo ndivyo miji inavyojengwa. Hakutakuwa na mfumuko wa bei za nyumba za ajabu ajabu. Watu wanaweza kupewa mikopo ya nyumba. Ukishindwa kulipa unatolewa tu hela yako uliyokwisha lipa hurudishiwi na nyumba anauziwa mtu mwingine.

Yafuatayo ni makampuni kumi kati ya mengi yanayoshughulika na ujenzi wa makazi ya wananchi nchini Marekani.

1. D.R Horton Inc.
2. Pulte Group (2013
3. Lennar Corp
4. Toll brothers Inc
5. Taylor Morrison Home
6. Hovnanian Enterprises.
7. KB Home
8. Ryland Homes
9. Standard Pacific corp
10. Meritage Homes

Mtu anitajie makampuni kumi ya ujenzi wa makazi (sio ya nyumba moja moja) yaliyopo Tanzania.

Inasikitisha sana viongozi wanaposafiri nje wanauona utaratibu lakini wanashindwa kuutekeleza Tanzania.

Hata ikibidi kuleta wawekezaji wa ujenzi wa miji. Watakuwa ni wa maana kuliko Acacia. Kwa sababu mwisho wa siku wawekezaji wa hivi wanatuachia miji ya kisasa.

Uwekezaji wa hivi utatoa ajira nyingi sana kwenye sekta ya ujenzi na usafi wa miji. Wawekezaji sio Tigo na Voda tu ambao tunawashukuru kwa kurahisisha mawasiliano lakini kwa upande mwingine wamebwetesha sana watanzania. Umbea umetawala kwenye instagram na Facebook. Kazi hakuna na wananchi wananyonywa sana visenti vyao kwenye mabando yasiyochacha na yanayochacha.
 
kwelii mkuu yatupasa kujifunz kupitia wenzetu na kupanua wigo ili vijana wapate ajira na kuijenga nchi yetu
 
NDUGU kila mtu akija hapa na alichoona Marekani au huko alikokuwa hii nchi itakuwa mkorogano kabisa. taifa lenye miaka 50 ya uhuru linalinganishwa kirahisi na US.
 
Kuna vitu umeviongelea haviendani...mosi suala la mikopo ya nyumba kwa wakazi - hili kwetu bongo halina uhakika kwani masharti ya mkopo mrefu 10years plus mtz wa kawaida ngumu kufikisha vigezo.

Miji au mitaa iliyojengwa na kampuni za ujenzi ipo ila haikaliwi na wana magomeni !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaongelea maisha ya magharibi ukilingamisha na Tanzania
Hivi unadhani ni rahisi kiasi hiko mtu wa kawaida akakope nyumba kisa tu imejengwa tabata

Tanzania mtu yuko radhi akakae bagamoyo imradi tu asisumbuliwe na mwenye nyumba
 
Hili wazo sio jipya. Kuna maeneo yaliyojengwa kwa mpangilio. Na mabenki yanatoa mikopo ya nyumba.

Kinachokosekana na utekelezaji mzuri. Unapoamua kujenga miji na makontrakta wajenzi wa kienyeji wapigwe marufuku kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea.

Mafundi wa reja reja wanafanya marekebisho tu kama kubadilisha sakafu au kuziba nyufa.

Bila ya kufanya hivyo hawa mafundi wa mitaani watazidi kujenga mabondeni tena kwa makusudi ili wenye nyumba walipwe fidia siku ya kubomolewa nyumba zao.
 
Na pia wataalamu wa ardhi wawe makini. Wasiwehuke tu mradi wamesikia kuna apartment zinajengwa wakakubali zijengwe Masaki na Oyster Bay. Yale ni maeneo ya viwanja vikubwa (low density) Apartment zikajengwe Magomeni, Ilala, Buguruni, Vingunguti. Tandika nk.
 
Mjengo mmoja wa nguvu kama huu unaweza kuchukua wakazi wote wa Magomeni. Na maeneo yatakayobaki yakafanyiwa miradi mingine.

dc49afbd0b08b4ab009d5e81462f96f6.jpg
 
Kweli tunajitendea haki mji mkuu wa Tanzania una maeneo ya hivi?
f69219c2aabe925bcf5edb090261b2fa.jpg
 
Benki hutoa mikopo ya kununua nyumba zinazofanyiwa ukaguzi wa ujenzi wake na thamani yake. Na pesa ya kununua nyumba hapewi mkopaji. Inalipia hiyo nyumba inayouzwa. Kwa kifupi benki inakununulia nyumba halafu unailipa. Hapo dhamana ni hiyo hiyo nyumba unayonunuliwa na benki.

Ni makosa makubwa kumpa mkopaji pesa taslimu akanunue kiwanja ajenge nyumba. Ndio maana mikopo ya Bongo unaweza kuomba mkopo wa nyumba ukaambiwa ulete hati ya nyumba nyingine iwe dhamana????????????
 
Sijawahi kusikia mtu Marekani kanunua kiwanja cha kujenga nyumba. Kwanza kuna majimbo mengine viwanja ni mali ya serikali. Nyumba yako kiwanja cha serikali. Utatia akili hapo.
 
Kuna vitu umeviongelea haviendani...mosi suala la mikopo ya nyumba kwa wakazi - hili kwetu bongo halina uhakika kwani masharti ya mkopo mrefu 10years plus mtz wa kawaida ngumu kufikisha vigezo.

Miji au mitaa iliyojengwa na kampuni za ujenzi ipo ila haikaliwi na wana magomeni !

Sent using Jamii Forums mobile app
Mixed economy ufanye kuwa katika kila uwekezaji kuwa na nyumba 10-20 ambazo ni affordable homes maana yake zinakuwa subsidies na serikali kwa akili ya wasio na uwezo.
Huwezi kuweka watu wenye income sawa sehemu moja lazima unahitaji service providers kama cleaners, supermarket attendants au restaurant waiters.
 
Nope, jamii zimegawika kwa kipato chao bila ya kuficha.
 
Si miujiza hii ndani ya miaka mia iliyopita Washington DC ilikuwa hivi:
be40bfd9c140f9ee4e1d659c98481a6d.jpg
 
Sijawahi kusikia mtu Marekani kanunua kiwanja cha kujenga nyumba. Kwanza kuna majimbo mengine viwanja ni mali ya serikali. Nyumba yako kiwanja cha serikali. Utatia akili hapo.
wapo mkuu una nunua land na ku design nyumba yako na unamwachia mpenzi huku wewe uk
 
Maono mazuri sana ila sio kwa serikali hii ya viwanda vya vyerehani vinne.

Sent using Jamii Forums mobile app

Serikali imeonyesha nia na muelekeo mzuri. Inahitaji ideas hasa za walioona nje kulivyo. Mimi kwenye hili suala la viwanda naona ingekuwa la wangeanza na kuleta mitrekta ya kulima na kuvuna mahindi na umwagiliaji mashamba nchi isiwe na shida ya chakula.
 
Huwajui wabongo. ..kwa tabia zao wanaona shida kukaa kwenye apartment.

Utakuta anaishi na bata. ..kuko gorofani bata watapandaje.

Kibustani cha tembele anakiweka wapi.
 
Back
Top Bottom